Na
Hadija Hassan, Lindi.
Bank
ya NMB wilayani Liwale imewatahadharisha wakulima wa zao la Korosho wanaotumia benk hiyo
kutotoa taarifa za kibenk kwa mtu yeyote kupitia njia ya simu.
Wito
huo umetolewa na meneja wa Benk hiyo wilaya ya Liwale Mkoani lindi Shamsi
Kashoro wakati wa mnada wa pili wa zao hilo wa chama kikuu cha ushirika cha
RUNALI kinachojumuisha Wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale Mkoani Lindi
uliofanyika katika kata ya likongowele wilayani humo.
Kashoro
alisema wakati huu wa msimu matapeli wengi wanatumia mwanya huo kujifanya wao
kuwa ni maofisa wa benki ili kuchukuwa taarifa za Wakulima na baadae kupata
mpenyo wa kuwaibia wakulima hao.
Kashoro
alieleza kuwa benk yao haitajihusisha na mawasiliano ya aina yoyote ya moja kwa
moja kwa njia ya simu na wakulima bali taarifa zote zinazohusiana na benk wakulima
watapata taarifa kutoka kwa viongozi wa vyama vyao vya Msingi AMCOS.
Hata
hivyo aliwasisitiza wakulima kuhakikisha wanaandika majina yao kwa usahihi
wakati wa kuandikisha korosho zao kwenye chama cha msingi AMCOS yakiwa
yanafanana na jina la akount anayotakiwa kulipiwa fedha zake ili kuondoa
usumbufu unaoweza kumcheleweshea Mkulima fedha yake.
Nae
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sara Chiwamba alitumia nafasi hiyo kuwaaasa wakulima
kuwa na nidhamu na fedha zao pamoja na kutumia fedha hizo kwa shughuli za kimaendeleo.
Kwa
upande wake mkulima wa korosho wa Wilaya ya Liwale Malima Evalist aliipongeza
Serikali kwa kuanzisha mfumo wa wazi wa ununuzi wa Zao hilo ambao unaweka uwazi
kwa wakulima na wanunuzi wa Zao hilo.
No comments:
Post a Comment