Bw.Emmanuel Kakwezi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Mkutano huo ulifanyika habari maelezo. |
By
Mwandishi wetu,
Wakala
wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) imesema katika kipindi cha miaka minne
ya serikali ya awamu ya tano chini ya
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli wameweza kupata
mafanikio mengi ikiwamo kutoa leseni na huduma zote za Brela kwa njia ya
mtandao.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema hii leo, Kaimu afisa Mtendaji Mkuu wa Brela Bw.
Emamnuel Kakwezi amesema mbali na kufanikiwa kutoa huduma za Brela kwa njia ya
mtandao pia, wa kushirikiana na COSTECH pamoja na shirika la miliki ubunifu
duniani (WIPO) wameweza kutekeleza mradi wa upatikanaji wa taarifa za
teknolojia zilizopo kwenye kanzidata za hataza (TISCs) kwa ajili ya kutumiwa na
watafiti na watumiaji wengine, jumla ya hataza milioni sabini na sita
(76,00,000) zinapatikana kwenye kanzidata husika.
Pia
katika kipindi hicho, brela imeweza kuanzisha utoaji wa leseni za kundi A na
kundi B kwa njia ya mtandao. Mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya malipo ya
serikali yaani Government electronic payment gateway (GEPG) na mfumo wa taarifa
ya mapato wa mamlaka za serikali za mitaa yaani Local Government Revenue
Collection Information System (LGRCIS).
Itakumbukwa
kuwa majaribio ya mfumo huo ulianza rasmi October 1, 2019 na mpaka sasa leseni
za Biashara Kundi A zilizotolewa na Brela na Leseni za Biashara kundi B katika
Manispaa ya Bukoba, Chalinze,Wilaya ya Karagwe, Mji wa Mafinga, Manispaa za
Ilala na halimashauri za Jiji la Mwanza zinatolewa kwa njia ya mtandao.
Akizungumzia
takwimu katika utoaji leseni kwa mfumo wa mtandao toka Octoba 1, 2019, jumla ya
leseni za biashara 1206 zimetolewa, kati ya hizo Brela imetoa leseni 470, Jiji
la Mwanza leseni 199, na Manispaa ya Ilala leseni 537.
Pia
brela imeweza kuanzisha dirisha la mfumo wa utoaji wa taarifa za kibiashara za
Kimataifa, dirisha hilo linamuwezesha mtumiaji au muombaji kufahamu taarifa
mbalimbali za upatikanaji wa leseni na vibali kwa bidhaa zinazouzwa nje na zinazoingizwa
ndani ya nchi.
Dirisha
hilo linatoa fursa kwa mwomabji kutembelea tovuti ya www.trade.business.go.tz
na kupata taarifa zote za kibiashara zinazohusiana na uuzaji wa biashara nje ya
nchi na ndani kwa ujumla wake (export and import process)
Kupitia
dirisha hilo mtumiaji atafahamu sharia, kanuni, taratibu, muda utakaotumika pamoja
na gharama za kila aina ya huduma (administrative procedures) atakaohitaji na
wapi apite ili kufanikisha upatikanaji wa huduma anayohitaji.
No comments:
Post a Comment