Na Omary Mngindo
WANACHAMA
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kijiji cha Diguzi Kata ya Matuli Morogoro vijijini
mkoa wa Morogoro, wamemuomba Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.
John Magufuli kufuatilia kura za maoni kijijini hapo.
Wakizungumza
na Waandishi wa Habari, Wakazi Maulid Lwambo, Ramadhani Makwangu, Amini
Jonathani na Aisha Mohamed wamesikitishwa na hatua ya kukatwa kwa mgombea
ambaye ameshinda kura za maoni Nassoro Ramadhani.
"Diwani
Luca Lumomo anatusumbua sana, huyu ni jamii ya mfugaji, hivyo anataka kutumia
nafasi yake kutaka kukiteka kijiji chetu kukifanya kiwe cha wafugaji, kwa kuwa
yeye ni mfugaji hivyo anatumia nafasi hiyo kutaka Mwenyekiti wa kijiji chetu
nae awe mfugaji," alisema Lwambo.
Amemuomba
Rais John Magufulo ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa aangalie figisu
hizo wanazofanyiwa kwani diwani wao amekuwa tatizo kubwa kwa maendeleo ya
kiniji chao.
Nae
Ramadhani anayetetea kiti hicho amesema kuwa anafanyiwa figisu hizo na uongozi
wa CCM wilaya wakishinikizwa na diwani wao Lumomo ambaye anatumia nafasi yake
ya udiwani kushinikiza ili mgombea wake Daud Ndukuye apite.
Amina
alisema kuwa figisu hizo zinazofanyika kwa mgombea ambaye ni chaguo lao
linatokana na shinikizo wanalompandikizia Ramadhani kwamba ameiingizia serikali
hasara kutokana na kukataa kwa mradi wa mpango wa urasimishaji ardhi kijijini
hapo.
Kwa
upande wake Lumomo amekanusha kujihusisha na figisu zinazotajwa, huku akisena
kuwa kulikuwa na ongezeko la wana-CCM siku moja kabla ya kufanyika kwa kura za maoni,
hatua iliyomlazimu mgombea was nafasi hiyo kupinga.
Katibu
Mwenezi wa chama hicho Mkoa wa Morogoro Anthony Mhando alisema kuwa taarifa
hizo anazisikia juu juu tu lakini hazijamfikia rasmi katika ofisi yake
No comments:
Post a Comment