Na
Shushu Joel
MAMLAKA
ya mapato Tanzania (TRA) imewataka wananchi kujenga utamaduni wa kuchukua
risiti kwa kila manunuzi wanayofanya kwa kuwa kutokuchukua risiti ni kosa
kisheria.
Akizungumza
na baadhi ya wateja katika moja ya vituo vya mafuta vilivyoko wilaya ya Kibiti
mkoani Pwani Mkurugenzi wa huduma ya elimu kwa walipa Kodi Richard Kayombo
alisema kuwa wananchi walio wengi hawachukui risti zao mara baada ya
kuhudumiwa.
Alisema
kuwa kitendo wanachokifanya ni hasara kwao kwani inaweza ikatokea kitu kibaya
katika biashara hiyo huku risiti uliacha kwenye kituo cha mafuta hivyo msaada
wako utakuwa ni mdogo sana ukilinganisha na ukiwa na risti.
"Nasikitika
sana kuona kuna ndoo iliyojaa risti zilizoachwa na watu ambao wamehudumiwa
mafuta, jamani risiti ni muhimu sana pia ni kosa kisheria kutokuchukua risiti
yako"Alisema Kayombo.
Kayombo
amesema kuwa Sheria ya usimamizi wa Kodi inatanabaisha kuwa mtu yoyote
asiyechukua risiti anafanya kosa kisheria na anaweza kutozwa faini kuanzia
shilingi 30,000 hadi 1.5ml au kwenda jela kifungo kisichozidi mwaka mmoja.
"Sheria
iko wazi kabisa lakini TRA tunawasisitiza wateja wote kudai na kuchukua risiti
kila wanaponunua bidhaa au kupata huduma", alisema.
Aidha
aliongeza kuwa mamlaka ya mapatoTanzania imeanzisha mfumo wa utoaji wa elimu
kwa mikoa miwili miwili ingawa kwa sasa tumeanza na mkoa wa Morogoro na Pwani
kisha baada ya hapo tutaenda mikoa mingine miwili kwa lengo la kuwaelimisha
wananchi.
Mbali
na hilo Kayombo amewasisitiza wananchi wote kulipa kodi ya majengo mapema ili
kuondoa usumbufu wa mwisho wa mwaka kama walivyozoea.
"Wananchi
wengi wamekuwa wakishindwa kuelewa ni kwanini wanasisitizwa kulipa kodi, jamani
Kodi ndio zinaleta maendeleo nchini hivyo mkilipa kwa uaminifu maendeleo
makubwa mtayaona "Alisema.
Pia
amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kupeleka maendeleo makubwa sehemu mbalimbali
kwa kusudi la wananchi kutambua thamani ya Kodi zao wanazolipa.
Naye
Juma Ally mkazi wa kibiti amewapongeza TRA kwa kujitoa kwa wananchi katika
kuwaelisha juu ya masuala ya kulipa kodi.
Aliongeza
kuwa wananchi mnapaswa mjitokeze kwa wingi ili muweze kuvuna elimu hii maana ni
ya muhimu sana kutambua kiwango chako cha ulipaji Kodi.
Kwa
upande wake Fatma Hamadi ni mmoja wa wafanyabiashara wa duka katika wilaya ya
Kibiti ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli kwa usimamizi
wake wa miradi kwa kuonyesha wananchi kile wanachokitoa kupitia TRA kukiona
katika uhalisia.
Aidha
amiopongeza mamlaka ya mapato nchini TRA kwa elimu wanayoitoa kwa jamii.
No comments:
Post a Comment