Kamishna
Msaidizi wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abeli Mtui akizungumza
na waandishi ofisini kwake ambao hawapo pichani waliotembelea hifadhi hiyo
kuhusu vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya
Mkomazi Abeli Mtui akiwaonyesha waandishi wa habari bwawa la Dindira lililopo
hifadhini humo ambalo linatumiwa na wanyama kwa ajili ya kunywa maji
ambao walitembelea.
Bwawa la Dindira lililopo hifadhini humo ambalo
linatumiwa na wanyama kwa ajili ya kunywa maji.
.........................................
HIFADHI ya Taifa ya Mkomazi iliyopo wilayani Same mkoani
Kilimanjaro imeeleza kwamba watatumia mavuvuzela na tochi zenye mwanga mkali
kuwafukuza wanyama wanaovamia makazi ya wananchi wakiwemo Tembo na kuwarudisha
kwenye hifadhi.
Hayo yalisemwa na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi kwenye
Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Abeli Mtui wakati akizungumza na waandishi wa
habari ambao walitembelea hifadhi hiyo.
Alisema kwamba watashirikiana pia na baadhi ya taasisi
binafsi ambazo zimebuni mbinu za kuwafukuza wanyama hao ikiwemo la wakulima
kufundishwa namna ya kuweka uzio wa mabati ambayo yanayopiga kelele na
imesaidia kwa asilimia kubwa.
Kamishna huyo Msaidizi wa Uhifadhi alisema wamefanya
jitihada zote huku akitoa wito kwa wananchi wazingatie na wanaona ufumbuzi
mkubwa ni yale maeneo ambayo yalikuwa ni mapitio ya wanyama kufanya matumizi
bora ya ardhi, rafiki yanayoendana na yasiwe ya kilimo au yale ya
kuchunga ili kupunguza mgongano wa kuharibu mazao.
“Kikubwa ni kutenga au kufanya matumizi bora ya ardhi
kwenye vijiji yale maeneo yenye historia ya kupita wanyama watu wayapangie
matumizi ambayo ni rafiki au matumizi yanayoendana na yasiwe ya kilimo au yawe
ya kuchungia ili kupunguza mgogano wanyama kuharibu mazao”Alisema.
Aidha alisema kwamba wana matumaini makubwa na kuna
mikakati wanaoiweka ili wasaidiane na viongozi wa vijiji katika kukamilisha
mipango bora ya matumizi ya ardhi ili maeneo yaliyo onekana ni mapito ya
wanyama yaweza kufanyiwa matumizi mazuri yanayoendena na uhifadhi wa wanyama
pori pia na matumizi ya mifugo kama malisho.
Alieleza pia kwamba hifadhi hiyo ni moja kati ya hifadhi
ambayo inapakana na Hifadhi ya Tsavo West ya Kenya na katika mfumo wa ikolojia
ya savo mkomazi kwa upande wa Kenya ndio eneo lenye idadi kubwa ya Tembo kwa
mujibu wa sensa miaka iliyopita kwenye huo mfumo kulikuwa na tembo 23000.
Alisema na mwaka 2014 hesabu ilifanyika na walionekana
tembo 60 na wao wamefanya sensa mwaka huu wakati wa kiangazi wamepata tembo
zaidi ya 1000 ina maana idadi kubwa ya tembo wameongezeka na hao tembo ni kwa
sababu hawana mipaka wanaotembea kwenye mfumo wa ikolojia na kipindi hicho
wamekuwa na tembo wengi ambao wamekuwa wakipita kwenye makazi ya watu.
“Hili linatokana na kwamba mara nyingi tembo eneo ambalo
amepita miaka ya zamana anatabia ya kupita tena kilichoonekana kwenye kipindi
cha kiangazi mapito ambayo yalikuwa ya tembo wanapita watu wamevamia na kuweka
makazi hata madhara makubwa yametokea”Alisema.
Hata hivyo alisema kwamba changamoto kubwa ni watu
wamelima karibu na hifadhi huku wakiwa hawajaacha hata mita moja na ndio
changamoto inapelekea kuwa rahisi tembo kuingia kwenye hayo maeneo na mashamba
na kufanya uharibifu mkubwa.
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Uhifadhi katika Idara
ya Utalii hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Benard Mgina amesema hali ya utalii
wageni wamezidi kuongezeka kwa sababu ukiangalia takwimu 2009 hadi 2010 wageni
854 wametembela hifadhi wageni wa nje walikuwa ni 419 na wa ndani 435.
Aliema utaona kuna utofauti mkubwa sana vile vile
ulkiangalia hesabu kutoka mwaka 2009 /2010 kwenda 2018 hadi 2019 kuna tofauri
kwa sababu 2009 /2010 ilikuwa wageni 854 lakini 2018/2019 wamepokea wageni 2930.
Afisa Mwandamizi huyo wa Uhifadhi wa Idara ya Utalii
alisema kwamba wageni ambao wamepokelewa kwa mwaka 2018/2019 kati yao wageni
728 kutoka nje na 2200 walikuwa wageni wa ndani kuna utofauti mkubwa sana.
No comments:
Post a Comment