Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana
na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu.
...................................
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekubali ombi la Serikali ya
Kenya la kuwapatia madaktari 500 kufuatia upugufu wa madaktari uliotokana na
mgomo nchini humo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
alisema kutoka na maombi yaliyotolewa, serikali imeandaa utaratibu kwa
madaktari wa kitanzania kuwasilisha maombi yao katika tovuti ya wizara ya afya
pamoja kufuata taratibu zingine kama watakavyoelekezwa.
Alizitaja sifa za anayetakiwa kuomba nafasi hiyo kuwa ni shahada ya
kwanza ya udaktari, mafunzo ya vitendo pamoja na kusajiliwa na Baraza
madaktari la Tanganyika na kutuma maombi hayo katika barua pepe; maombiyakazi@moh.go.tz kabla ya
Machi 27saa 10 jioni.
Aidha, waombaji wanatakiwa kuambatanisha wasifu wao, nakala za vyeti vya
taaluma na matokeo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha kuhitimu mafunzo kwa
vitendo pamoja na cheti cha usajili kutoka Baraza madaktari la
Tanganyika.
“Tanzania hatuna upungufu wa madaktari isipokuwa Serikali haina uwezo wa
kuajiri madaktari wote wanaohitimu, kwa kuwa kwa mwaka kuna wahimu 1200 wa
shahada ya kwanza ya udaktari na uwezo wa kuajiri ni 450 tu” alisema Ummy.
Hata hivyo, Waziri Ummy alisema kuwa ajira hizo hazitawahusu watumishi wa
umma, hospitali teule za halmashauri na mashirika ya hiari ambao wanalipwa
mshahara na serikali. Madaktari watakaokidhi vigezo na sifa watapewa mkataba wa
ajira wa miaka miwili.
Nchi ya Kenya inakabiliwa na upungufu wa madaktari kutokana na mgomo
ulioanza mwezi Desemba mwaka jana, ambapo madaktari hao wamekuwa wakaidai
nyongeza ya mshahara na marupurupu mengine.
Waziri
wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza kuhusu Kutangaza ajira za Madaktari wapatao
500 ambao watakwenda kufanya kazi nchini Kenya. Ajira hizo zitawahusu Madaktari
ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za
serikali.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini
Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment