Thursday, March 2, 2017

TAASISI YA AL KHAYRIYYA YAJENGA MSIKITI MKURANGA.


Msikiti uliojengwa na Taasisi ya Al Khayriyya katika Kitongoji cha Mwasani Kata ya Dundani Wilayani Mkuranga Mkoani  Pwani.
 Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Aboubakari Zubeir akizungumza katika uzinduzi wa Msikiti wilayani  Mkuranga.
...........................

Katika uznduzi  huo,  uliojengwa na Taasisi ya Al  Khairiyya,  katika kitongoji cha Mwasani  kata ya Dundani  Wilayani  Mkuranga, Nasaha  mbalimbali zimetolewa ambapo, Sheikh Mkuu wa Tanzania kupitia Baraza Kuu  la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mufti, Aboubakari   Zubeir, aliwataka waislamu  kuwa kudumisha umojawao  ili  waweze  kufanikisha mambo mbalimbali  ya kimaendeleo katika  uislamu na  jamii  kwa ujumla.

Mufti   Zubeir, alisema mifarakano katika  dini haileti manufaahivyo  aliwataka  waislamu  kuacha mifarakano na badala yake watengeze nguvu  za  pamoja  katika kuyaendea  yale  waliojiwekea katika mamboya  kheri.

 Alisema umoja unaleta mapenzi baina ya waislamu na  kuwasukuma kutekeleza miradi  ya maendelea kwa maslahiya uislamu na jamii nzimainayowazunguuka.
 
Msikiti huo umejengwa  katika  kituo  cha Costal Muslim Teachers Association (COMTA) Kilichopo  Kitongoji cha  Mwasani  kata ya  Dundani Wilayani Mkuranga  mkoa wa Pwani  ambapo Masheikh mbalimbali waliweza  kupata nafasi  ya  kuzungumza na  kutoa nasaha zao.

Katika Nasaha hizo masheikh hao  walisema  Waislamu wanaweza kufanikisha mambo yao kwa kuwa  kitu  kimoja, kujiwekea malengo, kuchangia  na  kutekeleza yale wanayokubaliana kwa ukweli na uwazi.

Akizungumza katika  uzinduzi huo  wa Msikiti, Sheikh Muharami Mziwanda, alisema Waislamu wakijiwekea mipango  madhubuti ya kufikia malengo yao wanaweza kufanikiwa kufanya  maendeleo mbalimbali  kwaajili  ya dini yao na jamii kwa ujumla.

Akielezea Changamoto zinazowakabili  waislamu hapa nchini alizitaja ni pamoja  na matibabu  ambapo alisema kuwa kuna baadhi  ya magonjwa ya aibu kwa  wanawake yanatibiwa na madaktari  wanaume na magonjwa ya aibu kwa  wanaume yanatibiwa na madaktari  wanawake jambo  ambalo ni kinyume na utaratibu wa uislamu.

Aliongeza kwa kusema kuwa,  ikiwa Waislamu watajiwekea malengo ya kujenga Hospitali  kila mkoa ni jambo linalowezekana kwa kuunganisha nguvu za pamoja na hatimae kufanikisha ili Madaktari waajiriwe na kupangiwa kazi  kwa  mujibu wa uislamu  ambapo  Magonjwa ya  aibu ya  wanawake yatibiwe na madaktari wanawake na magonjwa aibu ya wanaume yatibiwe na  Madaktari  wanaume.

Nae, imamu wa Msikiti wa Kichangani jijini Dar es Salaam, Sheikh Waidi Alhadi  Omari, aliwataka waislamu wasichoke kujitolea katika mambo ya kheri na kwamba wafanye hivyo kwakutaraji malipo kutoka kwa Mwenyezimungu Subhanahu Wataala na wala si vinginevyo.

Alisema  watu  wengi  wanfikiri maliponi kulkipwa pesa tu, bali ukweli ni kwamba malipo mazuri na yenyefaida ya milele ni kupata thawabu za Mwenyezimungu Subhaanahu Wataala ambae  yeye ni tajiri asiefirisika na dhamana yakeni milele.

Kutokana na hilo, aliwapongezaTaasisiya Al Khariyya kwa juhudi kub wa wanayofanya katika ujenzi wamisikiti na uchimbaji wa visima ili kuunusuru uislamu hasa katika maeneo ambayo yamesahaulika.

Akizungumza kwa niaba ya  Mwenyekiti  wa  Taasisi ya  Al Kayriyya ambao  ndio waliojenga  Msikiti huo, Sheikh  Zein  Alisema  nwaka 2016 wamefanikiwa kujenga  Misikiti 8 ndani na nje ya Dar es Salaam ambayo imejengwa  kwa   kuunganisha  nguvu za  Pamoja na kuwataka Waislamu kuiunga Mkono  Taasisi ya Al Khairiya ili  kufanikisha  Malengo yake  ya  kuupeleka mbele Uislamu.

Sheikh  Zeini ameongeza kwa kusema kuwa Taasisi ya Al Khairiyya kwa mwaka  huu imeshafungua misikiti  miwili  na  kwamba inatarajia kujenga  miskiti 12  mpakakufikia  mwisho  wa mwaka huu  2017.

Sheikh Zein alisema kuwa, Taasisi ya Al Khairiyya, ni Taasisi iliyojumuisha watu mbalimbali waliokusudia kujitoleakwa njia Mwenyezimungu, nakwamba kila mmoja katiyao amejiwekea malengo ya kuchangia maendeleo ya uislamu  na hiyo ndiyo siri ya kufanikisha malengo waliojiwekea.

Msikiti huo umejengwa Katika Kitongoji cha Mwasani kata ya Dundani, wilayani Mkuranga, ambao umekabidiwa kwa taasisi ya Costal Muslim Teachers Association (COMTA) utaondoa adha ya muda mrefu ya kukosa msikiti katika kituo hicho Elimu ya dini ya Kiislamu.

Katika Risala iliyosomwa katika ufunguzi wa Msikiti huo, COMTA imetoashukrani zake za dhati kwa Taasisi ya Al Khairiyya kwa kufanikishaujenzi wa Msikiti huo ambao kwa muda mrefu walikuwa wakitekeleza ibada ya swala kwenye miti ya mikorosho na miembe.

Aidha, katika Risala hiyo iliyosomwa na Ustadhi Aliy Kitengu, imesema pamoja na kupata msikiti huo kituo hicho bado kinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya kusomea (Madarasa) pamoja na mabweni yakulala wanafunzi.

Taasisi ya  Costal Muslim Teachers Association (COMTA) imesajiliwamwaka 2007 ambayo inajishughulisha na utoaji waelimu yadini ya kiislamu, na kwamba mpaka sasa ina wanafunzi  wanaolala hapo 60 na wa kutwa ni 50 Chini ya UsimamiziwaSheikh Shaabani Mbwela.

Muenekano wa Msikiti huo  uliojengwa na Taasisi ya Al Khairiyya, katika  Kitongoji cha  Mwasani  Kata ya Dundani  wilayani  Mkuranga  Mkoa wa Pwani.
Viongozi wa Taasisi ya Al Khayriyya walipokuwa  wakiwasili  katika eneo  la  Msikiti  Wilayani   Mkuranga.

Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abouubakari Zubeir  akiwa  ndani ya  Msikiti huo wakati  wa uzinduzi.

Viongozi waTaasisi ya Al Khayriyya, kutoka  kushoto ni  Katibu, Yasin Hemani, wa pili kushoto ni Mweka hazina,   Abdullatifu Fazaldin,  wa tatu ni  Mohamed Nasser  na  Seif  Yahya.

Kushoto ni  Maliki Ahmad na Abdulkarim Gurnah.

Kiongozi wa  kituo cha Costal Muslim Teachers Association (COMTA) Sheikh Shaabani  Mbwela.
Waumini waliohudhuria uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment