Friday, March 3, 2017

16 WASHIKILIWA NA POLISI PWANI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI / MAUAJI.


 Kamanda wa  Polisi  Mkoa wa  Pwani,  Kamishna Msaidizi wa  Polisi  (ACP)  Boniventure Mushongi.

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Makachero wa Jeshi  la  Polisi  Mkoa wa  Pwani wakishirikiana na  wale kutoka  Makao Makuu ya Polisi, tunamshikilia  Khalid Mohamed (29) ambae ni fundi ujenzi na mkazi wa kwa Mathias Wilaya ya  Kibaha akiwa na Silaha aina ya SMG na risasi 14.

Mtuhumiwa huyo, tulimkamata huko eneo la Misugusugu Kata ya Misugusugu na Tarafa na Wilaya ya  Kibaha akiwa na Silaha hiyo aina ya SMG ambayo namba zake zimefutwa pamoja na risasi 14  jana Tarehe 02/03/2017 majira ya 17:15  HRS.

Mtuhumiwa huyo,  mb ali na  kukutwa na Silaha hiyo, pia alikutwana  risasi  4 za Shotgun, Mlipuko mmoja, Sime  moja, maski moja na koti moja vyote vikiwa vimehifadhiwa kwenye mfuko wa Rambo chini ya Ardhi kwenye Shamba la mtu  aliyejulikana kwa jina  moja  la Swai.

Uchunguzi  wa Awali umeweza kubaini kuwa, mtuhumiwahuyo na wenzake wengine 15 ambao tunawashikilia wamekiri kujihusisha na matukio ya uporaji kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa  Pwani,  likiwemo  tukio  la mauaji ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya  Liwale mwaka 2012-2016,  Ephraim  Mfingi  Mbaga (54) aliyuwawa  akiwa nyum bani kwake baada ya kupigwa risasi  kwenye  paja lamguu  wa  kushoto na kujeruhiwa kwa  kitu chenye ncha  kali ambapo alipoteza maisha akiwa njiani akipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.

Imetolewa na:-
Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Pwani
Boniventure Mushongi (ACP)
03 March 2017.      

No comments:

Post a Comment