Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikagua
gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja
wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017
kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya
maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
..............................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewasili mjini Mbabane –
Swaziland leo 16-Mar-2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu
wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC).
Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III
mjini Mbabane – Swaziland, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa
na Viongozi mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma wa
Serikali ya Swaziland Owen Nxumalo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili uwanjani hapo
amekagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kushuhudia vikundi
mbalimbali vya burudani uwanjani hapo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA kwenye
mkutano huo.
Hapo kesho tarehe 17-Marchi-2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atahudhuria mkutano wa Wakuu na Serikali wa
Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika
ambao utajadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika nchi za Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.
Mkutano huo wa SADC Double Troika utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo
ya mkutano wa Mawaziri wa Kamati Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika Dar
es Salaam tarehe 24 februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha ipo haja ya
kuitisha mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama kwenye
hizo.
Mkutano wa SADC Double Troika utahusisha nchi Sita wanachama wa asasi
hiyo ambazo ni Tanzania,Swaziland, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na
Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa
Dakta Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbabane – SWAZILAND.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia
vikundi vya Burudani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa
Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march,16, 2017 kwa
ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya
maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwasili Heshima kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa
III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano
wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC)
ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Swaziland alipowasili kwenye Uwanja
wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017
kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya
maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment