NAPE AMSHUKURU RAIS, APONGEZA UTEUZI WA MWAKYEMBE.

na3
Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewataka Watanzania kukubaliana na suala la  kusitishwa kwake uteuzi wa cheo hicho.

Akizungumza na waandishi nje ya Hoteli ya Protea, leo. Nape amesema wanatakiwa kukubaliana na hali halisi.

Rais John Magufuli amemteua Dk Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi hiyo ya Nape.

“Mkubali Tanzania ni kubwa kuliko Nape na hampaswi kuanzisha matatizo. Tanzania ni nchi yetu sisi na tujue Nape hawezi kuwa mkubwa kuliko Tanzania.

“Nawashauri kuwa watulivu, namshukuru Rais Magufuli kwa kunipa nafasi ya kufanya naye kazi kwa mwaka mzima.

“Nilifanya kazi yangu kwa akili na nguvu zangu zote. Nawashukuru wasanii, waandishi, wanamichezo kwa ushirikiano wenu.

 Nilipenda kuendelea kufanya kazi nanyi lakini muda wa aliyeniteua umefika, nitawakumbuka sana, ninawapenda sana,” alisema Nape.

Wakati anataka kuondoka katika eneo hilo, gari lake lilizuiwa na RPC wa Kinondoni, Suzan Kaganda hali iliyosababisha taharuki hadi Nape aliwapowaomba waandishi kuondoka eneo hilo ili naye aondoke.
 na4na1

Baadhi ya maaskari wakiwa wameimarisha ulinzi katika eneo hilo.
 na5na6

Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.