MBUNGE WA KYELA, ASHUHUDIA KUINGIZWA MAJINI KWA MELI YA MV. RUVUMA.

unnamed
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Kyela, Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe,  akishuhudia zoezi la kuingizwa majini kwa Meli mpya ya pili ya mizigo iitwayo MV Ruvuma kwenye bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, Mkoani  Mbeya.
............................
Tukio hilo la kuiingiza Meli hiyo limefanyika Machi Mosi, 2017 katika Bandari ya Itungi wilayani Kyela Mkoani Mbeya.

Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba mizigo zaidi ya tani 1000 inaungana na Meli nyingine mpya MV Njombe yenye uwezo wa kubeba zaidi ya tani 1000 ambayo iliingizwa majini siku tano zilizopita.

Meli zote mbili zipo kwenye hatua ya mwisho ya utengenezaji na majaribio kabla hazijaanza rasmi kubeba mizigo kwenye ziwa Nyasa.

Tayari wateja mbalimbali wamejitokeza kutaka mizigo yao ianze kubebwa yakiwemo makampuni yanayojishughulisha na biashara ya makaa ya mawe.

Meli hizo mbili za mizigo za kisasa zenye uwezo wa kubeba tani elfu moja (1,000) za mizigo kila moja,  zimegharimu shilingi bilioni 11.


Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.

KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU