Rais wa chama cha soka cha Madagascar Ahmad Ahmad ameshinda kiti cha Urais wa Shirikisho la Soka Afrika katika uchaguzi uliofanyika leo March 16, 2017.
Uchaguzi uliomalizika Addis Ababa umempa ushindi Ahmad Ahmad baada ya
kupata kura 30 dhidi ya 20 za Issa Hayatou.
Matokeo hayo yanahitimisha miaka 29 ya utawala wa Hayatou kama kiongozi
wa juu wa soka la Afrika.
Mipango na mbinu kabla ya uchaguzi zimepelea kuwashangaza wengi baada ya
kushuhudia kambi ya Hayatou ikidondoshwa.
Hayatou mwenye miaka 70 sasa, alikuwa rais wa CAF tangu mwaka 1988 wakati
huo Lionel Messi akiwa na miezi tisa tu tangu azaliwe wakati mtawala huyo
mzaliwa wa Cameroon alipotangazwa kusimamia soka la bara la Afrika.
Alianza kutawala tangu March 10, 1988 alikuwa anaifukuzia rekodi ya
kuendelea kusalia madarakani kwa awamu ya nane mfululizo.
Uchaguzi ulifanyika leo baada ya mkutano mkuu wa 39 huko mjini Addis
Ababa.
Ahmad, who appeared very emotional, becomes only the seventh Caf
president in the body’s 60-year history.
Ahmad anakuwa rais wa saba wa CAF kwenye historia ya shirikisho hilo
lenye miaka 60 hadi sasa tangu kuanzishwa kwakwe.
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Afrika Issa Hayatou.
No comments:
Post a Comment