Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya
Muheza, (aliyevaa juba kulia)
akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wanawake wajasiriamali wakati alipofungua
jukwaa la wanawake mkoani Tanga hivi karibuni.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
MhandisiMwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, kulia akipata
maelekezo kutoka kwa mmoja wa wanawake wajasiriamali wakati alipofungua jukwaa
la wanawake mkoani Tanga hivi karibuni.
............................
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo ameziagiza wilaya
zote za mkoa huu kuunda majukwaa ya wanawake kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo
ili yaweze kuwa chachu ya
kuwakomboa kimaendeleo na kiuchumi.
kuwakomboa kimaendeleo na kiuchumi.
Mhandisi Mwanasha ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza aliyasema hayo
hivi karibuni wakati akizindua jukwaa la wanawake mkoani Tanga ambalo
litakuwa na malengo makuu ya kuwainua na kuwawezesha wanawake.
kiiuchumi lililofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Alisema uwepo wa majukwaa hayo itasaidia kutoa fursa kwa wanawake kuweza
kushiriki kikamilifu kwenye masuala mbalimbali ikiwemo kuwepo na majukumu ya
kuwawezesha wanawake kuweza kujiinua kiuchumi
kutokana na shughuli wanazozifanya zikiwemo za ujasiriamali.
kutokana na shughuli wanazozifanya zikiwemo za ujasiriamali.
Aidha pia aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuzalisha bidhaa bora
na wenye kiwango cha kimataifa ili waweze kupata nafasi ya kuziuza ndani na nje
ya nchi ili kuwasaidia kuongeza pato lao na Taifa
kwa ujumla.
kwa ujumla.
“Wajasariamali warasimishe biashara zao ili ziweze kutambulika kisheria
ikiwemo kulipa kodi lakini pia muachane na suala la kujiingiza kwenye biashara
haramu ambazo zinaweza kukatisha ndoto zenu “Alisema.
“Kupitia Jukwaa hili mnaweza mnalitumia kusaidia wanawake kujikwamua
kiuchumi na kuweza kufia sera ya asilimia 50 kwa 50 hivyo ili kufikia huko
jukumu lenu kuonyesha uwezo lakini pia wekezeni kwenye elimu kupitia mkusanyiko huu “Alisema.
Awali akizungumza Mjasiriamali wa kampuni ya kutengeneza Fenicha, za
majumbani na maofisini mkoani Tanga Edna Boimanda aliwashauri wanawake kuunganisha nguvu
za pamoja ili kuona namna ya kuanzisha benki ya wanawake kwani hiyo ndio fursa
ya kipekee wanayoweza kujikwamua kiuchumi.
Alisema kupitia benki hiyo itawawezesha waanawake kujiletea maendeleo kwa
kupata mikopo itakayokuwa chachu ya kufikia malengo yao ya kupata mafanikio.
Aliwataka kutumia fursa hiyo ya kutengeneza misingi ya kibiashara ambayo
inaweza kuwasaidia kuondokana na changamoto ambazo wanakumbana nazo kwenye masuala ya
mitaji.
Naye kwa upande wake Mjasiriamali wa Kikundi cha Raha Gani Women
Group Haifa Kijazi aliiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia
viukundi mbalimbali ili viweze kujikwamua kiuchumi.
Group Haifa Kijazi aliiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia
viukundi mbalimbali ili viweze kujikwamua kiuchumi.
“Kwani
ukiangalia leo hii vikundi vingi vimekuwa msaada
mkubwa kuwa mkombozi wa wanawake kwa kuwawezesha kukabiliana na ugumu wa maisha kwa
kuwekeza na kukopa “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment