Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akikabidhiwa ripoti ya
uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia
Kituo cha Televisheni cha Clouds Media na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa
sakata hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan
Abbass, Tarehe 22 Machi 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya uchunguzi wa tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
kuvamia kituo cha Televisheni cha Clouds Media ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass (kushoto) akimwelezea Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye ushahidi wa CCTV
uliombatanishwa katika CD aliyomkabidhi jana Tarehe 22 Machi 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma
za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha
Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Dkt. Hassan Abbass.
...........................
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
amepokea taarifa ya kina kuhusu chanzo, sababu na namna tukio la Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda alivovamia kituo cha Utangazaji cha Clouds
Media akiwa na walinzi wenye silaha Machi 17, 2017.
Akipokea taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa
Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan
Abbas ameishukuru Kamati kwa utulivu wao na kuifanya kazi hiyo kwa
utaalamu na umakini mkubwa huku jamii ikitaka matokeo kwa haraka.
Aidha Mhe. Waziri amesema kuwa ripoti hiyo ataiwasilisha kwa mamlaka
husika kwa ajili ya uamuzi na maelekezo.
“Nimeipokea ripoti na ninawahakikishia kuwa nitaikabidhi ripoti hii kwa
wakubwa zangu wao ndo wenye mamalaka ya kufanya chochote”,Alisema Mhe. Nape.
Kamati aliyoiunda Mhe Waziri ilikuwa na wajumbe wanne ambao ni
Bw.Deodatus Balile kutoka Jamhuri,Bw.Jesse Kwayu wa Gazeti la The Guardian,Bibi
Nengida Johanes wa Upendo Media na Bibi Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Dkt.Hassan Abbas.
Katibu
wa Kamati ya Kuchunguza Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi
za Kituo cha Televisheni cha Clouds Media, Deodatus Balile akielezea yaliyomo
katika ripoti yao kabla ya kumkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Nape Moses Nauye (kushoto) jana Tarehe 22 Machi 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye (katikati) akifafanua
jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya
uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia
Kituo cha Televisheni cha Clouds Media janaTarehe 22 Machi 2017 Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia
ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari –
MAELEZO Dkt. Hassan Abbass na Katibu wa Kamati hiyo Deodatus Balile.
No comments:
Post a Comment