Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,
imemuachia huru Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema (CHADEMA) kwa
dhamana ya shilingi milioni moja pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho
vinavyotambulika na serikali.
Mbunge
Lema alikaa mahabusu kwa takribani miezi minne akikabiliwa na kesi ya
uchochezi, katika Gereza Kuu la Arusha lililopo Kisongo, na kwamba amefanikiwa
kupata dhamani na kupokewa na washabiki wake waliomtandikia kanga ili apite
wakati akitoka mahakamani hapo.
Hukumu
hiyo ndogo imesomwa na jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Fatuma Magimbi katika mahakama kuu Arusha.
Akizungumza
nje ya mahakama hiyo, Lema alisema kuwa amejifunza mengi alipokuwa mahabusu kwa
kipindi chote hicho na kwamba ameandaa waraka wa kumwandikia Raisi kuelezea
yale aliyoyaona alipokuwa mahabusu.
Nae
mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alisema kuwa wanamkaribisha tena
Lema bungeni na kwamba kamati ya chama imemaliza vikao vyake mjini hapa na
kuwashukuru wabunge wa mikoa mbali mbali waliofika kutetea dhamana ya lema.
No comments:
Post a Comment