Thursday, March 23, 2017

RIPOTI YA KAMATI YA NAPE.

NOKO 1
Katibu wa Kamati ya Kuchunguza Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi za Kituo cha Televisheni cha Clouds Media, Deodatus Balile akielezea yaliyomo katika ripoti yao kabla ya kumkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nauye (kushoto) lana Tarehe 22 Machi 2017 Jijini Dar es Salaam.
.................................



RIPOTI YA KAMATI ILIYOUNDWA NA WAZIRI NAPE NNAUYE KUHUSU UVAMIZI WA CLOUDS MEDIA.

Waziri Nape Nnauye anapokea taarifa ya kamati aliyoiunda kuhusu uvamizi katika kituo cha utangazaji cha Clouds.

Tulifanya mahojiano na wafanyakazi 14 wa kituo cha Clouds.-Balile
Tulifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Mkoa, tulimpigia simu lakini hakupokea.- Balile 

"Hata tulipofika katika ofisi yake, aliondoka kupitia mlango wa nyuma". -Balile

"Baada ya kushindwa kuonana naye, tukajiridhisha kuwa amechagua mwenyewe kutotumia fursa ya kuhojiwa". -Balile 

"Katika uchunguzi wetu, tumejiridhisha kuwa Mkuu wa Mkoa alivamia kituo cha Clouds akiwa anaendesha gari mwenyewe". -Balile

"Kamati imejiridhisha kuwa RC na askari wenye silaha waliingia hadi ndani ya studio iliyokuwa ikirusha matangazo". -Balile 

"Kamati imejiridhisha pia kuwa palikuwa na vitisho kwa walinzi na wafanyakazi kwa kutumia askari wenye silaha". -Balile 

"Miongoni mwa vitisho ni kuwalazimisha kurusha kipindi vinginevyo angewaingiza kwenye tuhuma za dawa za kulevya". Balile

"Baada ya hapo aliwatisha kuwa yote yaliyotokea usiku ule, yabaki pale pale ndani" - Balile 

"Tumejiridhisha kuwa RC Mkuu wa Mkoa aliingilia taratibu za uhariri kwa kulazimisha habari anayoitaka iruke" - Balile

"Kamati haikuona uthibitisho wowote kuwa kuna wafanyakazi waliopigwa na vitako vya bunduki au kupigwa mitama" - Balile 

MAPENDEKEZO YA KAMATI.

"Pendekezo la kwanza, Mkuu wa mkoa aombe radhi Clouds na kwa wanahabari wote" - Balile 

"Pendekezo la pili, Waziri husika atoe taarifa kwa mamlaka husika ili Mkuu wa Mkoa achukuliwe hatua " - Balile

"Pendekezo la 3, ni vyombo vya usalama kufanya uchunguzi juu ya askari kuingia Clouds na silaha za moto" - Balil

#RipotiYaUvamizi

No comments:

Post a Comment