Wednesday, March 8, 2017

TaSUBa YAPONGEZWA KWA IGIZO LA DAWA ZA KULEVYA.



Vijana wa TaSUBa wakionyeshauwezo  wao wa  kuigiza namna jamii invyoathirika na Dawa za kulevya.
 ............................
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo TaSUBa imepongezwa  kwa kuandaa igizo linaloonyesha madhara yatokanayo na madawa ya kulevya kwa jamii.

Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na Kamishna wa Kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini, Rogers  Sianga alipokuwa akizungumza katika kituoa cha  Life and Hope SOBA-Bagamoyo.

Alisema ujumbe uliotolewa na TaSUBa kwa  njia ya maigizo ni uhalisia wa matatizo yanayoikumba jamii pale watu wanapotumia Dawa za kulevya.
Aliongeza kwa kusema kuwa ni vyema  kikundi hicho cha sanaa kikapewa umuhimu wapekee  katika kutoa elimu juu ya madhara ya  matumizi ya Dawa za kulevya  ili jamii ijifunze kupitia igizo hilo.

 Alisema ujumbe unaotolewa kwa  njia ya  sanaa unafika kwa haraka zaidi  ukilinganisha  na kuuweka kwenye maandishi hivyo katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya ni muhimu pia kutumia kikundi hiki cha sanaa ili kufikisha ujumbe.

 Nae katibu wa  Baraza  la viongozi  wa dini  nchini  John Solomon alisema kikundi hicho cha sanaa kinapaswa kusaidiwa katika kuhakikisha ujumbe  unafika kwa jamii.

Aidha, alitoa wito kwa jamii  kudhamini utengenezaji  wa CD ya  igizo hilo ili isambazwe ujumbe ufike kwa urahisi.

No comments:

Post a Comment