Kamanda
wa polisi mkoani Pwani,kamishna msaidizi mwandamizi ,Onesmo Lyanga,wa
kushoto,akizungumza jambo.
.................
JESHI la polisi mkoani Pwani ,limewabaini baadhi ya mtandao wa watuhumiwa
wa mauaji yanayoendelea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji wapatao kumi na
mbili akiwemo mwanzilishi wa mauaji Abdurshakur Ngande Makeo .
Aidha jeshi hilo linaendelea na msako kuwatafuta watu hao ambao wanne
picha zao zimepatikana .
Akizungumzia hali ya kiusalama ya Mkoa kutokana na vitendo vya mauaji
vinavyoendelea katika wilaya hizo ,Kamanda wa polisi mkoani hapo,Onesmo Lyanga
,alisema wanaendelea na mapambano na upelelezi kuwapata wahusika wote .
Alieleza ,jeshi la polisi limewabaini kwa majina na picha kwa baadhi yao
.
Kamanda Lyanga ,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Faraj Ismail Nangalava
,Anaf Rashid Kapera @Kapelo ,Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa .
Wengine ni Shaban Kinyangulia ,Haji Ulatule ,Ally Ulatule ,Hassan Uponda
,Rashid Salim Mtulula ,Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame .
Kamanda Lyanga ,alieleza kwamba ,Saidi Ngunde inadaiwa anaishi Ikwiriri
na Omar Abdallah Matimbwa anaishi Dar es salaam ambapo picha zao wanazo pamoja
na ya Faraj na Anaf .
Alieleleza wengine nane bado picha zao hazijapatikana hadi sasa .
“Jeshi letu limebaini hayo kwa kushirikiana na wasiri wetu huku
tukiendelea na uchunguzi zaidi ” alibainisha .
Kamanda Lyanga alisema ,watuhumiwa hao ,wamegundulika kuwa hupendelea
kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga ,kisiwa cha Saninga kijiji cha
Nchinga .
Kamanda huyo ,alifafanua kijiji kingine ni cha Mfesini kata ya Nyamisati
na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti ,Rufiji na Mkuranga.
Jeshi hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa siri kufichua
watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama kimkoa .
Limetangaza bingo ya kumpatia sh. mil .tano yeyote atakaefanikisha zoezi
hilo .
Hivi karibuni jeshi hilo lilitangaza kuwa kuna mtandao wa majina ya
wauaji 102 ambao wanawasaka hadi sasa ili kudhibiti vitendo vya mauaji vinavyotia
hofu wananchi .
Picha za wauaji wanaosakwa Pwani:
No comments:
Post a Comment