Raia nane kutoka nchi ya Ethiopia wamekutwa wamefariki katika kijiji cha
Amani makolo taarafa ya kingonsera wilayani mbinga mkoani wa ruvuma
huku wengine 25 wakiwa hai wanashikiriwa na jeshi la polisi.
Habari kutoka jeshi la polisi mkoa wa ruvuma kupitia kaimu kamanda wa
polisi ACP DISAMASI KISUSI zinasema raia hao wa Ethiopia walikuwa wanasafirishwa
kwenda nchi ya AFRIKA KUSINI kupitia Upande wa MALAWI mwa ziwa NYASA.
Vifo vya Waithiopia hao vinatokana na kubebwa kwenye kontena la lori
wakitokea NAMANGA, ARUSHWA hivyo kutokana na hali mbaya ya hewa hali zao
zilianza kubadilika na kupelekea kufariki.huku miili ya marehemu hao ikiwa
imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya MBINGA.
Jeshi la polis mkoa wa ruvuma kwa kushirikiana na jeshi la uhamiaji
linaendelea na uchunguzi kubaini walioleta miili ya marehemu na wale
wasiliokamatwa hatua za kisheria zitafuatwa.
No comments:
Post a Comment