ASKARI
wa usalama barabarani wilayani Kibaha mkoani Pwani wakisikiliza elimu juu ya
matumizi ya mfumo wa kubaini stika bandia kwa magari mbalimbali,mfumo
ulianzishwa na mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA
kamishna
wa mamlaka ya usimamizi wa bima nchini,dr.Baghayo Saqware ,wa kwanza kulia
akieleza jambo kwa askari wa usalama barabarani eneo la Mailmoja Kibaha
Jopo
la wajumbe kutoka mamlaka ya usimamizi wa bima nchini wakihakiki stika za bima
katika moja ya lori eneo la mizani Mailmoja Kibaha.
............................
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA),imeanza kampeni endelevu ya
kuhakiki magari yenye stika za bima bandia ili kuondoa wimbi la stika hizo
ambalo hulisababishia serikali kukosa mapato.
Aidha zoezi hilo litawezesha kubaini mtandao wa makampuni yanayotengeneza
stika hizo .
Akizindua zoezi hilo mjini Kibaha,kamishna wa mamlaka ya usimamizi wa
bima nchini,dr.Baghayo Saqware ,alisema kampeni hiyo itaendeshwa kwa kusimamiwa
na jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kwa kushirikiana na
TIRA.
Alieleza kwamba ,uhakiki huo utafanyika kwa kutumia mfumo wa teknolojia
ya TEHAMA-unaoitwa TIRA –MIS .
Saqware alisema,askari wa usalama barabarani wanapaswa kutumia mtandao na
ujumbe wa kawaida kwenda namba 15200 ambapo watapokea maelezo ya halisi ya
stika anayoikagua.
Hata hivyo alibainisha kuwa,wameamua kubuni mfumo huo ili kukomesha wizi
unaofanywa na baadhi ya makampuni yanayotengeneza stika na wamiliki wa magari.
Kamishna huyo alisema,tatizo hilo linaweza kukua zaidi endapo mamlaka
hiyo itaendelea kukaa kimya ikiwa ni watengeneza wakuu wa stika hizo za bima.
“Tatizo ni kubwa hasa mikoa inayopitiwa na barabara kuu ya Dar es salaam
,Pwani na Arusha”
“Kutokana na hilo tumeona vyema tukaanza kujenga ufa kabla ya ukuta ,Hali
isije kuwa mbaya zaidi’alisisitiza Saqware.
Saqware alielezea,wamezindua zoezi na kampeni hiyo rasmi kwa kuanzia
wilaya ya Kibaha kwa kutoa elimu kwa askari wa usalama barabarani juu ya mfumo
huo.
Alisema kila ofisi yao ya kanda itatekeleza zoezi hilo kwa kutoa elimu
kwa wananchi,askari wa usalama barabarani na madereva.
Nae kamanda wa usalama barabarani mkoani Pwani,Abdi Issango ,alisema
zoezi hilo limeanzishwa katika muda muafaka kwani utitiri wa stika feki ni kero
kubwa.
Alisema wimbi la stika bandia linakwamisha mapato ya serikali na kuumiza
wananchi wasio na hatia.
Kamanda Issango ,itasaidia kukamata magari yenye stika feki ili kubaini
mtandao wa makampuni mbalimbali yanayotoa bima zisizo halali.
“Watu waliokuwa wakiuziwa bima
bandia, kwa sasa watauziwa bima halali na watapata haki zao bila usumbufu “ “Kuna kesi nyingi za bima feki ama wamiliki wengine hutumia stika moja ya
bima kwenye magari yake zaidi ya kumi,kinyume na taratibu za TIRA”alifafanua
Issango.
Kamanda Issango ,alisema bima ni kinga ya ajali ,wahanga wanatakiwa
kufidiwa hivyo kama gari limepata ajali halijakata bima linamnyima
mwananchi haki yake ya matibabu,majeruhi na kifo.
Alisema kwa mkoa wa Pwani hali hairidhishi ,kwani magari mengi yamekuwa
yakifoji ,na kuwa na stika walizozipata kwa njia za mkato.
Kamanda Issango ,alitoa wito kwa wananchi hasa wamiliki wa mabasi,malori
na magari binafsi kuacha kupitia njia zisizo halali kununua ama kutengeneza
stika bandia .
No comments:
Post a Comment