Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
WAKATI serikali ikijipanga kuanzisha Mkoa wa kipolisi katika wilaya ya
Rufiji, Kibiti ,Mafia na Mkuranga ,katibu wa CCM kata ya Bungu ,wilaya ya
Kibiti, Halife Mtulia amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kibiti, Zena Mgaya, alisema
marehemu ameuawa majira ya saa 4 usiku may 13 .
Alisema alipata taarifa la tukio kutoka kwa viongozi wa CCM kata.
Zena alieleza Mtulia ameuawa akiwa anatoka uwani mwa nyumba yake kwenda
kuoga akiwa ameshika ndoo ya maji ndipo wauaji wawili walipojitokeza na kumuua
kisha kutokomea kusikojulikana.
“Wauaji hao
walitumia usafiri wa pikipiki kwa kuiacha mbali na eneo la tukio na baada ya
kutimiza adhma yao walitembea kuifuata walipoipaki kisha kuondoka “alielezea
Zena.
Alisema Marehemu alikuwa Katibu wa CCM Kata ya Bungu, Mjumbe wa Mkutano
mkuu wa CCM Taifa kutoka wilaya ya Kibiti na mjumbe wa Serikali ya kijiji
Nyambunda na ameacha mke na watoto.
Zena alisema
kufuatia matukio ya mauaji kijiji cha Nyambunda kata ya Bungu kimeshapoteza
Mwenyekiti wa kiiji, Mtendaji wa Kijiji, na wenyeviti watatu wa vitongoji
vilivyoko katika kijiji hicho .
Alipoulizwa
kuhusiana na uchaguzi wa ndani ya chama unavyoendelea ngazi ya shina na matawi
Zena alisema wanachama wanagomea kujitokeza.
“Uchaguzi wa
safari hii ni mgumu hakuna anaejitokeza kugombea kabisa, watu wanahofu
“alifafanua.
Nae Asha
Hemed na Ramadhani Swedy walisema hali bado ni mbaya kiusalama katika wilaya
hiyo na Rufiji.
Walisema
jeshi la polisi lisambaze askari wake na maeneo ya vijijini ambako wahalifu hao
ndio wamejikita huko.
Matukio hayo ni pamoja na Jan 19,ambapo mjumbe wa serikali ya kijiji cha
Nyambunda ,Oswald Mrope, aliuawa kwa kupigwa risasi.
March 1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said
Mbwana aliuawa.
Octoba 24,2016 afisa mtendaji wa kijiji cha
Nyambunda Ally Milandu alipigwa risasi na kufa na novemba 6,2016 .
Tukio jingine ni lile la mwenyekiti wa kitongoji cha
Nyang’unda kijiji cha Nyambunda Mohammed Thabiti alipigwa risasi akielekea
kwake.
Jeshi la polisi Pwani limethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kudai , linaendelea kupambana na kuwasaka wahalifu na kuimarisha
ulinzi.
No comments:
Post a Comment