Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara wa nchi za Afrika
Kusini na Tanzania uliofanyika Alhamisi Mei 11, 2017 Jijini Dar es Salaam,
ambao ulijadili fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara zilizopo baina ya
Mataifa hayo.
.............................
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wafanyabiashara na wawekezaji wa
Afrika Kusini kujitokeza na kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ina mazingira
yaliyo salama, bora na fursa wezeshi.
Rais Magufuli ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini mkutano wa wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliojadili fursa na vivutio vya uwekezaji katika mataifa hayo.
Rais Magufuli ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini mkutano wa wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliojadili fursa na vivutio vya uwekezaji katika mataifa hayo.
Rais Magufuli amesema Tanzania
ina vivutio mbalimbali vya uwekezaji vyenye kutoa fursa kwa wafanyabiashara na
wawekezaji kutoka Afrika Kusini kuwekeza katika sekta yoyote nchini kwani
uwekezaji huo una uhakika wa kuzaa matunda mazuri.
“Napenda kuwahakikishia
wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza Tanzania kuwa nchi hii ina amani tangu
tupate uhuru mnamo mwaka 1961,ina mazingira mazuri ya kibiashara,utulivu wa
kiasiasa pamoja na uchumi unaotabirika hivyo nawasihi wafanyabiashara wa Afrika
Kusini kuwekeza nchini kwetu,”alisema Dkt. Magufuli.
Ameongeza kuwa Tanzania ina
soko kubwa la kuuzia bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kwani tumezungukwa na
nchi nane ikiwemo ya Burundi, Congo, Malawi, Rwanda, Uganda na Zambia kwa kiasi
kikubwa zinashirikiana na Tanzania katika kufanya biashara za kimataifa hivyo
wakiwekeza Tanzania watapata soko la nchi nyingi.
Kwa upande wake Rais wa Afrika
Kusini. Jacob Zuma amesema kuwa wamekubaliana na Rais Magufuli kukuza
ushirikiano hasa wa kiuchumi wa nchi zote mbili ikiwa ni moja ya kichocheo
kitakachosaidia kuleta faida na kutunza ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya
nchi hizo mbili.
“Hadi sasa kuna zaidi ya
Makampuni 200,000 kutoka Afrika Kusini ambayo yamewekeza nchini Tanzania katika
sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo, mawasiliano, sekta za fedha, ujenzi,
madini na utalii lakini kwa kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya kuwezesha
ukuaji wa uchumi tunaamini kampuni hizo zitaongezeka,”alisema Rais Zuma.
Ametoa rai kwa nchi hizo mbili
kuacha kujikita katika bidhaa pekee kwani sio endelevu na haitengenezi ajira za
uhakika na badala yake kuwekeza nguvu katika uzalishaji.
Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akibadilishana mawazo na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF) Reginald Mengi na
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye NA Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Biashara (TNBC), Mhandisi Raymond Mbilinyi wakati wa mkutano wa
Mkutano wa Wafanyabiashara wan chi za Afrika Kusini na Tanzania uliofanyika
Alhamisi Mei 11, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli na mwenyeji wake, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma wakifuatilia
kwa makini hotuba za Viongozi mbalimbali wa Serikali za nchi hizo wakati wa
mkutano wa Wafanyabiashara wa Mataifa hayo uliofanyika leo Alhamisi Mei 11,
2017 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wafanyabiashara kutoka nchini Afrika Kusini wakifuatilia kwa makini hotuba
za Viongozi mbalimbali wa Serikali za nchi hizo wakati wa mkutano wa
Wafanyabiashara wa Mataifa hayo uliofanyika leo Alhamisi Mei 11, 2017 Jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza jambo na Rais Dkt. John Pombe Magufuli
wakati wa mkutano wa Wafanyabiashara wa Mataifa hayo uliofanyika Alhamisi Mei
11, 2017 Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment