Mkuu
wa TAKUKURU Wilaya ya Bagamoyo, Raymond Katima, akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
..............
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilaya
ya Bagamoyo, imetoa somo kwa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Bagamoyo
kuhusu vitendo vinavyoashiria mazingira ya Rushwa kwenye idara mbalim bali
katika Hlmashauri.
Akitoa somo hilo mbele ya Madiwa, na wakuu wa
Idara mbalimbali ndani ya ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mkuu wa TAKUKURU
Wilaya ya Bagamoyo, Raymond Katima alisema kukosekana kwa maadili miongoni mwa
watendaji ndiyo chanzo cha Rushwa katika Halmashauri.
Alisema watendaji wa Halmashauri na Madiwani wapo
kwaajili ya kuwatumikia wananchi hivyo uadilifu na uwajibikaji ni nguzo muhimu
katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Aliongeza kuwa katika utekelezaji wa Miradi ya
maendeleo ya jamii kwenye Halmashauri mazingira ya Rushwa yanajitokeza hasa pale wahusika wanapokosa
uzalendo na kupindisha sheria na kanuni
katika kutangaza Zabuni, uandaaji wa muswada wa makadirio ya kazi, Bill of
quantities (BOQ) na kuchelewesha malipo kwa mkandarasi hata pale ambapo kazi
imekamilika na kukaguliwa.
Alisema mazingira ya Rushwa yanapojitokeza kwenye
utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya jamii hupelekea miradi hiyo kutekelezwa
chini ya kiwango kwasababu y a kulinda
maslahi ya watu wachache na hatimae
Halmashauri kupata hasara na Taifa kwa ujumla.
Aidha, alisema kuwa, ili kuhakikisha Malengo ya
Miradi ya M aendeleo yanafikiwa kwa
kupitia sera ya Serikali ya Uwazi na Utawala wa Ushirikiano (Open Governance Partnership), Halmashauri
inapaswa kuweka wazi fedha zinazoletwa na Serikali au wafadhili ili wananchi
wajue kiasi kilicholetwa na hatimae wahoji pale Mradi unapokamilika chini ya kiwango ukilinganisha na fedha
zilizoletwa.
Akizungumzia mazingira yanayopelekea Rushwa
katika sekta ya Afya, Katima alisema wapo baadhi ya madaktari, manesi na
wauguzi ambao hutengeneza mazingira ya rushwa kwa mgon jwa.
Akielezea hali hiyo, alisema Daktari, Nesi au muuguzi hujikwepesha
kumuhudumia mgonjwa licha kumuona na kujua tatizo lake hali inayopelekea mgonjwa
kulazimika kutoa chochote ili apate matibabu kwa haraka jambo ambalo ni
kinyume cha sheria na kwamba hiyo ndiyo
Rushwa.
Akifafanua neno Rushwa Katima alisema, Rushwa ni Fedha au kitu chochote cha thamani
kinachotolewa na kupewa mtu mwe nye madaraka ili atimize au asitimize wajibu wake kwa maslahi yamtoaji au mpokeaji.
Kwa upande wao, Madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo
wamempongeza mkuu huyo wa TAKUKURU wilaya na kuomba elimu hiyo ifike
k wenye kata zao na kushuka hadi
ngazi ya vijiji ili jamii yote iwe
na uelewa kuhusu viten do vya rushwa na hatimae vita dhidi rushwa iwe ya watu wote.
Mkuu huyo wa TAKUKURU wilaya ya Bagamoyo, aliwataka wananchi wote kutoa ushirikiano na
Taasisi hiyo ili
kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa katika Halmashauri ya Bagamoyo.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt . Shukuru Kawambwa na Diwani wakata ya
Magomeni, Mwanaharusi Jarufu wakimsikiliza
mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Bagamoyo akitoa
mada kuhusu Rushwa.
Wakuu
wa idara za Halmashauri ya
Bagamoyo wakisikil iza kwa makini mada
ya Rushwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo Ali Ali
Issa wa kwanza kushoto, wa pili kushoto
ni Makamo mwen yekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamed Usinga,
Kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Zinga,
Mohamed Mwinyigogo ,katikati ni Diwani wa kata ya Kiromo Hassan R. Usinga (Wembe) na wa kwanza kulia ni Diwani wa kata ya Kisutu, Awesu Ramadhani.
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Bagamoyo, Fatuma Latu katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo Ali Ali
Issa wa kwanza kushoto, ni Makamo mwen yekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamed Usinga.
No comments:
Post a Comment