nyumba ikiwa imeangukiwa na mti kama
inavyoonekana
katika picha
katika picha
mvua
inayonyesha mfululizo Mkoani Arusha imeleta maafa makubwa katika familia
ya mzee Jonathani Kalambiya{55} mkazi wa sokoni II katika kijiji cha
kinyeresi wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya mti
mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.
mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.
Mkasa
huo wa usikitisha ulitokea jana majira ya saa 7 usiku baada ya mti huo kung’olewa
na maji uliangukia nyumba hiyo iliyokuwa jira na mti huo.
Kamanda
wa polisi Mkoani Arusha, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo alithibitisha tukio hilo na
kuwataja watoto waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na watoto wawili
wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni mlinzi wa hospital ya ya Dr Mohamed ya Jijini
Arusha.
Mkumbo
aliwataka wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya tukio
alikuwa kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa kidatu cha pili
wa shule ya sekondari ya Inaboishu.
Kamanda
alimtaja mwanafunzi mwingine ni ambaye ni mtoto wa mzee huyo ni Grolia
Jonathani(11) mwanafunzi wa shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani Arumeru
Mkoani Arusha.
Amesema
watoto wengine wa mzee huyo ni pamoja na mtoto wa kwanza wa mzee huyo aliyetambuliwa
kwa jina la Giliad Jonathani(31),Lazaro Lomnyaki
(26) na Best Jonathani(20).
(26) na Best Jonathani(20).
Kamanda
Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana uliangukia
nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji
la Arusha na Mkoa kwa ujumla.
Alisema na
kuitakia pole sana familia yam zee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa
sana kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu katika
wakati huu mgumu kwake.
Kamanda Mkumbo
ametoa wito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukuwa tahadhari katika kipindi
hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha
kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.
Amesema
kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga mengine
hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukuwa tahadhali hiyo.
Aidha
kamanda ametoa tahadhari kutokana na habari za uzushizinazoendele kuwa jana
kwenye kuaga miili ya wanafunzi kuna mtu alidondoka juu ya mti na kufariki
pamoja na mama mmoja mtoto wake mdogo alifariki,amesema habari hizo siyo za
kweli wananchi wazipuuze kabisa
No comments:
Post a Comment