TAREHE 14.05.2017 MAJIRA YA SAA
02:00HRS USIKU KATIKA KISIWA CHA GANA KILICHOPO KIJIJI CHA KAMASI KATA YA
ILANGALA WILAYA YA UKEREWE, MTU ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA MKAMA MGENGELE, MIAKA
36, MVUVI NA MKAZI WA GANA KISIWANI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA
LA KUMFANYIA UKATILI MTU ANAYEDAIWA KUWA MPENZI WAKE AITWAYE ESTER LAZARO MIAKA
37, MHUDUMU WA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO BACELONA NA MKAZI WA GANA
KISIWANI, KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI KWENYE KIGANJA CHA MKONO WAKE WA
KUSHOTO HADI KIKAANGUKA CHINI KISHA AKAMKATA TENA KWENYE PAJA LA MGUU WA KULIA,
KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA NA
MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA BI ESTER LAZARO KWA MUDA MREFU, LAKINI HIVI KARIBUNI
WALIKUWA KWENYE MGOGORO WA KIMAPENZI, INASEMEKANA KWAMBA TAREHE TAJWA HAPO JUU
MTUHUMIWA ALIFIKA KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO BACELONA AMBAPO MPENZI
WAKE BI ESTER ANAFANYIA KAZI HUKU AKIWA AMELEWA POMBE NA KUANZA KURUSHIANA
MANENO MAKALI.
INADAIWA ILIPOFIKA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MTUHUMIWA ALIMWENDEA BI
ESTER LAZARO HUKU AKIWA HAFAHAMU KINACHOENDELEA NA KUMKATA KWA KUTUMIA KITU
CHENYE NCHALI KWENYE KIGANJA CHA MKONO WAKE WA KUSHOTO HADI KIKAANGUKA CHINI
KISHA AKAMKATA TENA KWENYE PAJA LA MGUU WA KULIA KISHA AKAONDOKA ENEO LA TUKIO.
WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI
KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA JUU YA TAARIFA
HIZO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA. MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA
JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MAJERUHI
AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA UKEREWE AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI
YAKE INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA
WA MWANZA AKIWAOMBA KUACHA TABIA YA KUJICHULIA SHERIA MKONONI KWANI MADHARA
YAKE NI MAKUBWA LAKINI PIA NI KOSA LA JINAI.
AIDHA ANAWAOMBA WANANDOA AU WATU
WALIOKUWA KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI KWA MUDA MREFU WAKIWA KWENYE MIGOGORO
WAENDE POLISI KIPO KITENGO CHA DAWATI AMBACHO KINAWATAALAMU
WANAOSHUGHULIKIA MATATIZO HAYO AU WAENDE KWENYE TAASISI NYINGINE ZA SERIKALI
KAMA USTAWI WA JAMII NA SIO KUJICHULIA SHERIA MKONONI.
KATIKA TUKIO LA PILI;
MNAMO TAREHE 14.05.2017 MAJIRA
YA SAA 18:30HRS JIONI KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SHINYANGA KIJIJI CHA
NYANG’HOLONGO TARAFA YA USAGARA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA
T.571 BHU AINA YA MINBUS FUSO MALI YA MOHAMEDI MAMDALI LIKITOKEA MWANZA KWENDA
KAHAMA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FREDY KAWASANGE
MIAKA 39, MKAZI WA KAHAMA, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE JUMA NKANU,
ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI YA 40 HADI 50, NA MKAZI WA KIJIJI CHA
IBONGOYA “A” NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA
ANAVUKA BARABARA BILA KUCHUKUA TAHADHARI YEYOTE HUKU AKIWA AMELEWA NDIPO
GHAFLA ALIKUTANA NA GARI TAJWA HAPO JUU LIKIWA KWENYE MWENDO KASI NA KUGONGWA
NA KUPELEKEA MAREHEMU KUPOTEZA MAISHA.
DEREVA WA GARI HILO AMEKAMATWA YUPO
KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA
MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHI HOSPITALI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA
AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA
MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU PINDI
WAWAPO BARABARANI AKIWATAKA KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI WOTE
ILI KUJIEPUSHA NA AJALI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA PIA ANAWATAKA
WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA
BARABARANI WAKATI WOTE ILI KUWEZA KUZUIA AJALI ZISIZO ZA LAZIMA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
No comments:
Post a Comment