Chama Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu
matukio ya Mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkutanga na Rufiji
Mkoani Pwani ili kuepusha mauaji hayo kuendelea kutokea.
Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi, HUMPHEY POLEPOLE, amesema hayo Jijini Dar es salaam
leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji yanayoendelea
katika Wilaya hizo.
POLEPOLE pia
amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinaelekeza akili, nguvu zao
katika Wilaya hizo kwa kuwa maujia hayo yanasababisha kuzorota kwa shughuli za
maendeleo.
Amesema chama kwa
muda mrefu kimekaa kimya kikiamini hatua zitachukuliwa kwa kuwa wanachama wake
na watendaji wameendelea kupoteza maisha ambapo amesema kwa sasa imetosha.
Kuhusu suala la uchaguzi ambao unaendelea ndani ya Chama hicho amesema
mauaji hayo yanakiweka Chama katika mazingira magumu ya kufanya chaguzi zake
hivyo ni vema hatua zikachukuliwa sasa.
Katika hatua
nyingine, POLEPOLE amesema Chama kimeipongeza Kamati Maalum ya kuchunguza
Mchanga wa Madini kwa kazi nzuri iliyofanywa sanjari na kuwaomba wananchi
kumuunga mkono Rais JOHN MAGUFULI kwa hatua alizozichukua kwa watendaji
kutokana na Ripoti ya Mchanga wa Madini.
No comments:
Post a Comment