Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kushoto)
akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina
kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya
wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya
habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.
Mwanasheria
kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia
(kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi
katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Wanatasnia hao wa habari
wamepata fursa ya kujadiliana kwa pamoja na LSF namna vyombo vya habari
vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii.
Baadhi
ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya
habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa
Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia
taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.

Wakili
Harold Sungusia akisisitiza jambo alipokuwa akiwasilisha mada kwa baadhi ya
wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na
LSF.
Baadhi
ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada anuai.
Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Robart
Zephania (mbele aliyesimama) akizungumza katika semina hiyo.
No comments:
Post a Comment