KAIMU
Katibu wa Jumuia ya Umoja wa Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa
Shaka Hamdi Shaka, akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama na watendaji wa serikali katika Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.
....................................
Na
Omary Mngindo.
Chalinze.
KAIMU
Katibu wa Jumuia ya Umoja wa Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa
Shaka Hamdi Shaka ameziagiza Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kwenda
kujifunza uendeshaji wa shughuli zao katika halmashauri ya Chalinze namna ya
kuwatumikia wananchi wao.
Shaka
ametoa kauli hiyo Mei 10 alipokuwa akizungumza na viongozi wa Halmashauri hiyo,
Madiwani, watendaji mbalimbali pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM
Wilaya ya Bagamoyo chini ya Mwenyekiti Almass Masukuzi, Katibu Kombo Kamote,
Mwenyekiti wa Halmashauri Said Zikatimu, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Chalinze, Edes Lukoa na viongozi wengine.
Kauli
ya Shaka imefuatia taarifa iliyotolewa na Zikatimu kuhusiana na namna
ilivyotekeleza majukumu yake katika kipindi cha miezi minane tangu kuanzishwa
rasmi mwezi wa saba mwaka 2016 ikitokea Bagamoyo ambapo katika kipindi hicho
imefanikiwa kuwalipa posho ya sh. 30,000 Wenyeviti wa vijiji wapatao 64.
"Mbali ya kuwalipa posho
Wenyeviti wetu, pia kuanzia Julai Mosi mwaka 2016 tunasafirisha bure wagonjwa
wote wanaopewa uhamisho kimatibabu kutoka kwenye Zahanati, Vituo vya afya na
Hospitali ambao hawalipi hata sentano, mbpo awali walikuwa wanachangia sh.
60,000 kwa ajili ya mafuta wanapotoka eneo moja kwenda lingine," alisema
Zikatimu.
Kuhusu
ujenzi wa Zahanati katika vijiji vyote, Zikatimu alisema kwamba wameshaanza
zoezi hilo katika baadhi ya vijiji na kwamba imani yao ni kuwa kila kijiji
kitapata zahanati yake ikiwa ni kuunga mkono sera ya Serikali Kuu ya kutaka
kila kijiji kuwa na Zahanati na Vituo vya afya ngazi za Kata.
"Sanjali na hayo tumeweza
kurejesha asilimia 10 ya makusanyo yetu ya ndani kwa vijana na wanawake, zaidi
ya sh. Mil. 160 tumekopesha vikundi pia tunataraji wakati wowote tutakwenda
tena kugawa hundi kota ya nne, hayo ni mafanikio ya urejeshwaji wa asilimia
hiyo ambapo Wenyeviti na wananchi wanasimamia vema mapato," alisema
Mwenyekiti huyo.
Aidha,
Shaka alianza kwa kuwapongeza viongozi hao huku akisema ni mfano wa kuigwa na
kwamba viongozi wa Halmashauri zote, Manispaa na Majiji nchini kwenda Chalinze
kujifunza namna ya ukusanyaji mapato na Utawala bora na kwamba wametekeleza kwa
vitendo azima ya Rais Dkt. John Magufuli ya kuwataka viongozi kuwatumikia
wananchi wao katika kuwapatia maendeleo.
"Niwaombe waandishi andikeni
hili, nawataka Maofisa wote wa Halmashauri, Majiji na Manispaa zote nchini kuna
Chalinze kujifunza namna ya ukusanyaji mapato kwani wamejiongoeza wenyewe
katika kuwalipa posho Wenyeviti, nimetembea nchi nzima ndio kwanza mambo haya
nimeyakuta hapa," alisema Shaka.
No comments:
Post a Comment