Mkuu
wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama na mbunge wa viti maalum mkoani Pwani
Subira Mgalu mwenye kiremba cha blue wakitembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa
za wajasiriamali wa Mji wa Kibaha ,baada ya kuzindua jukwaa la wanawake la
kuwawezesha kiuchumi mjini hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi )
....................
WILAYA ya Kibaha imezindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi na
kuchagua viongozi wake watakaoongoza katika kipindi cha miaka mitano.
Jukwaa hilo limempitisha Betty Msimbe kuwa mwenyekiti huku Sada Duda
akichaguliwa katibu kipindi hicho .
Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leah Lwanji
aliwataja viongozi hao ambao wamechaguliwa na akina mama wajasiriamali
mbalimbali .
Alieleza kuwa kuundwa kwa jukwaa hilo kutasaidia kuwezeshwa vikundi vya
akinamama wajasiriamali kirahisi .
Leah alisema wanawake waungane waache kujiweka binafsi ili kupiga hatua
kimaendeleo na kiuchumi .
Hata hivyo alisema ,katika kipindi cha mwezi april hadi may mwaka huu
halmashauri ya Mji huo imechangia sh .mil 56 kwa kukopesha vikundi 34 vya
wanawake ,kwenye kata 14 zilizopo mjini humo .
Leah alielezea kwamba ,July hadi desemba mwaka 2016 ,walitoa mil .16 kwa
vikundi Tisa na Jan – march mwaka 2017 wametoa mil.70 kwa vikundi 46 .
Alisema kwa upande wa fungu la vijana afisa maendeleo huyo ya jamii
,wametoa asilimia kumi katika mapato ya ndani kwa kutoa sh.mil 32 zilizopelekwa
saccos ya vijana .
“Tunamkabidhi mkuu wa wilaya ya Kibaha hundi ya sh.mil 56 kutoka NMB
itakayogawiwa katika vikundi 34″ alisema Leah .
Nae diwani wa viti maalum Mji wa Kibaha ambae pia ni katibu wa jukwaa la
uwezeshaji mkoani Pwani ,Elina Mgonja alisema ,umoja wao utawawezesha kuwa na
sauti kupigania fursa za kiujasiriamali .
Alisema wamejipanga kuthubutu kuanzisha miradi mbalimbali na kushikana
mkono ili kujikwamua kimaisha .
Elina alitoa rai kwa wanawake kujitambua na kujithamini .
Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,aliwataka wanawake
wathubutu kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa kwenda na sera ya uchumi wa
viwanda .
Aliwaomba wajenge tabia ya kugombea nafasi za uongozi bila kuwaachia
wanaume .
Assumpter alisema kinamama waamke waache kulala kwani sio wakati wa
kuzorota na kusemana majungu na kukatishana tamaa .
No comments:
Post a Comment