Umoja
wa watanzania Ujerumani UTU e.V watingisha jiji la Essen nchini Ujerumani baada
ya kufanya mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba ulioandamana na sherehe za
ushindi wa viongozi wapya.
jijini Essen katika ukumbi wa Bob’s Cafe,
watanzania zaidi ya 75 ambao wanaishi nchini humo walihudhuria mkutano huo ili
kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wao.
katika safu ya uongozi
mpya Mhe Mfundo Peter Mfundo alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa umoja huo
baada ya kukosa mpinzani. Makamo mwenyekiti mpya ni Mhe Salim Malumbo Jr.
Katibu mkuu ni Julieth Myn, muweka Hazina ni Bi Nashe Mvungi, Mkaguzi wa
mahesabu namba 1 ni Mhe Bi Jovither Mushashu, Mkaguzi wa mahesabu namba 2
ni mhe Bi. Lilian Sorogo. Mjumbe namba Moja ni Mhe Ebrahim Makunja aka
Kamanda Ras Makunja na Mjumbe namba 2 ni Mhe Vanessa Lymo.
Pamoja na mengi
yalioongelewa kwenye mkutano huo azma ya umoja wa watanzania Ujerumani
UTU e.V ni kuwaendeleza watanzaniawanaoishi hapa ujerumani na hata kuwaletea
maendeleo watanzania wanaoisho Tanzania, umoja ni Nguvu na utengano ni Udhaifu
No comments:
Post a Comment