Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Fatuma Omari Latu, akiangalia
msimamo wa Halmashauri yake katika usafi wa mazingira kupitia mradi wa Nipo
Tayari chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwenye
semina inayofanyika mjini Morogoro.
Mratibu wa mradi wa usafi wa mazingira uitwao Nipo Tayari Juliana
Kitira akimuonyesha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Kigoma, Elinatha
Elisha takwimu za hali ya usafi wa mazingira katika halmashauri yake kwenye semina
inayofanyika Morogoro.
Mradi huo pia unahamasisha uwepo wa vyoo bora na kunawa mikono na maji
safi baada ya kutoka chooni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Simanjiro mkoani Manyara Yefred
Myenzi akiapa kuwa yupo tayari kutekeleza kwa vitendo kampeni ya nchi nzima ya
usafi wa mazingira iitwayo Nipo Tayari kwenye semina inayofanyika mjini
Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Sabas Damian
Chambasi akiapa kuwa yupo tayari kutekeleza kwa vitendo kampeni ya nchi nzima
ya usafi wa mazingira iitwayo Nipo Tayari kwenye semina inayofanyika mjini
Morogoro.
.......................
Halmashauri
za wilaya zimetakiwa kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maji kwa
kuchangamkia fursa ya fedha za kitanzania bilioni 250 zilizotolewa na Shirika
la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID) kwa ajili ya utekelezaji wa mradi
wa usambazaji maji safi na salama vijijini (2016-2020).
Mkurugenzi
Msaidizi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Injinia Jackson Mutazamba aliwaambia
wakurugenzi Halmashauri za wilaya katika semina inayofanyika mjini Morogoro, kuwa ni halmashauri
chache tu ndio zimeanza kupata fedha hizo mara baada ya kukidhi vigezo
vinavyotakiwa na wafadhili.
“Kuna
fedha za kutosha katika mradi huu ukilinganisha na mwamko wa Halmashauri katika
kuchangamkia fursa hii ya kuongeza mtandao wa maji katika maeneo yao,” alisema
na kuongeza kuwa, fedha hizo zinaweza kuzisaidia halmashauri kuanzisha miradi
mipya na kukarabati ile ya zamani ili iweze kutoa maji kwa wakati wote wa
mwaka.
Alisema
moja ya sharti la upatikanaji wa fedha hizo ni ufanisi katika utekelezaji wa
miradi iliyopita na ubora wa ripoti za kila mwezi kama ambavyo programu hii
inavyozitaka halmashauri.
Alisisitiza kuwa, Kigezo hicho ni muhimu sana katika kuvuka hatua moja
hadi nyingine na kupata fungu kubwa zaidi la fedha ambalo litawezesha
kutekeleza miradi mikubwa zaidi katika Halmashauri husika.
Alisema Halmashauri zinaweza kupokea aina mbili za malipo kama vile paundi za
kiingereza 50 kwa ajili ya kuendeleza kituo cha maji na kwamba kiasi hicho kinaweza
kuongezeka hadi paundi 1,500 kulingana na ufanisi wa utekelezaji katika hatua
ya mwanzo.
“Ukipata
paundi zaidi ya 1,500 kwa mara moja kwa miradi ya vijijini ni nyingi sana
katika kuiboresha na kuifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuhakikisha
upatikanaji wa maji wakati wote.
Na pia fedha hizi zinaweza kutumika kuanzisha
vituo vipya vya kusambazia maji hivyo kufanya mtandao wa maji kuwa mkubwa zaidi
katika eneo husika,” alisema.
Alibainisha kuwa,
ni Halmashauri 57 tu ambazo ziliweza kuvuka vigezo viwili vya mwanzo kwa mwaka
jana na kuweza kupata fungu kubwa zaidi la kiasi cha paundi za uingereza 5,000,
fedha ambazo kwa miradi ya maji vijijini zinaweza kusaidia sana katika
upatikanaji wa maji wakati wote wa mwaka.
Aidha, aliwahimiza
wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya kuchangamkia fursa hiyo ya fedha kwa ajili ya kutekeleza
miradi mingi ya maji na kuifufua ile iliyokufa iweze kufanya kazi tena na
kuongeza mtandao wa maji kuwa mkubwa zaidi ili kufikia azma ya serikali ya
asilimia 95 wa watu wanaopata maji katika miaka michache ijayo.
Injinia
Mutazamba aliongeza kwa kusema kuwa, lengo la kuwakutanisha wakurugenzi wote nchini
katika semina hiyo ni kuweza kuwaeleza kwa kina kuhusu fursa hiyo ya fedha za
wafadhili ambazo bado zipo nyingi na zinaweza kusaidia kupunguza na hata
kumaliza kabisa tatizo la maji hasa sehemu za vijijini.
Alisema
programu hiyo ya kuongeza mtandao wa maji vijijini unatekelezwa kwa ushirikiano
kati ya shirika la kimataia la DFID la uingereza na serikali ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment