Mkuu wa jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro akizungumza na
waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua mbalimbali za kudhibiti
masuala ya uhalifu likiwemo la mauaji yanayoendelea Kibiti leo jijini Dar es
Salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari pamoja na Makamanda wa Jeshi la Polisi
wakimsikiliza IGP Mpya, Simon Sirro alipokuwa akizungumza na Wanahabari mapema
leo jijini Dar es Salaam
............................
Mkuu wa Jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro ameahidi kutoa
sh.milion 10 kwa yeyote atakayetoa taarifa za kufanikisha kuwakamata watu
wanaofanya mauaji ya viongozi huko Kibiti wilayani Rufiji Utete mkoani Pwani.
Akizungumza leo na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sirro amesema kumekuwa na mauaji ya
wananchi na Askari katika Wilaya ya Rufiji Utete pamoja na Wilaya ya Mkuranga
ambayo yamekuwa yakifanywa na wahalifu wachache kwa malengo wanayoyajua wao.
Amesema Jeshi la Polisi
bado linaendelea na Operesheni mbalimbali kuhakikisha kwamba vitendo hivyo
haviendelei kuweza kubaini mzizi.
Aidha Mkuu wa Jeshi la
Polisi Mpya amezungumzia juu ya waendesha boda boda kuwa na tabia ya kukaidi
kufata sheria za usalama barabarani ikiwemo kubeba abiria zaidi ya mmoja
‘mishikaki.
Sirro amesema waendesha
bodaboda wanashindwa kufuata sheria za usalama barabarani kwa kupita taa
nyekundu pamoja na kutovaa kofia ngumu ‘Helment’ ambapo kumesababisha wengine
vifo na majeruhi ya kuwafanya kuwa na ulemavu wa kudumu.
Hata hivyo amesema
kumekuwa na malalalamiko dhidi ya baadhi ya Askari polisi kujihusisha na
vitendo vya rushwa lakini pia baadhi ya wananchi kuwashawishi Askari kupokea
rushwa ikiwa ni sehemu ya ngao ya kukwepa kuwajibishwa pindi wanapokuwa
wamefanya makosa.
No comments:
Post a Comment