- MAJAMBAZI WATATU WAMEUAWA NA KUPATIKANA KWA SILAHA MBILI WILAYANI NYAMAGANA
KWAMBA TAREHE 19.05.2017 MAJIRA YA SAA 02:30HRS
USIKU KATIKA VIWANJA VYA ST. MARY’S MTAA WA NDOFE WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA
MKOA WA MWANZA, WATU WATATU WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WANAOFAHAMIKA KWA
MAJINA YA
1.BENEDICTO THOBIAS @ BENE MIAKA 31, MKAZI WA NYAMATARA BUHONGWA,
2.MABULA SEGEJA @ BULA, NA 3.CHARLES THOMASI GARULA WALIJERUHIWA KWA RISASI NA
BAADAE KUFARIKI DUNIA WAKATI WAKIPELEKWA HOSPITALI BAADA YA WAKIRUSHIANA RISASI
NA ASKARI POLISI, AMBAPO KATIKA TUKIO HILO ASKARI WALIFANIKIWA KUKAMATA SILAHA
MBILI 1.BASTOLA AINA YA DUTY CZ 75P -07 YENYE NAMBA B.512637 IKIWA NA RISASI 15
NA MAGAZINI 2 NA 2.SHORT GUN ILIYOFUTIKA NAMBA IKIWA NA RISASI MBILI NA MAGANDA
MAWILI YA RISASI.
AWALI ALIKAMATWA MGANGA WA KIENYEJI AITWAYE AYUBU
NYAMWERU MIAKA 45 MKAZI WA KATORO MKOANI GEITA, AKIWA NA LAPTOP TATU MBILI AINA
YA HP NA MOJA AINA YA ASUS NA SIMU MOJA AINA SUMSUNG AMBAYO ILIIBIWA KATIKA
TUKIO LA KUVUNJA NYUMBA USIKU NA KUNYANG’ANYA MALI AMBAZO NI LAPTOP TATU, SIMU
MBILI NA SILAHA AINA YA BASTOLA DUTY CZ 75P-07 NA FEDHA, TUKIO HILO LILILOTOKEA
TAREHE 13.05.2017 KATIKA MAENEO YA NYAMONGOLO NA KUFUNGULIWA KESI YENYE KUMBU
NAMBA NY/IR/3773/2017.
MTUHIMIWA HUYO AYUBU NYAMWERU ALIHOJIWA NA ASKARI NA
KUTAJA WENZAKE ANAOSHIRIKIANA NAO KATIKA KUFANYA MATAKIO YA UVUNJAJI NA
UNYANGA’ANYI HAPA MWANZA NA MAENEO MENGIINE LIKIWEPO TUKIO LA UJAMBAZI
LILILOLIELEZA HAPO JUU NA MENGINE.
ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA TAARIFA HIZO
NA KUMKAMATA BENEDICTO THOBIAS @ BENE NA KUWEKA MTEGO SEHEMU TAJWA HAPO JUU
AMBAPO WALIPANGA NA WENZAKE WAKUTANE ILI KWENDA KUTELEZA UHALIFU WALIOKUWA
WAMEUPANGA.
AIDHA USIKU WA TAREHE 18.05.2017 MAJIRA YA SAA
2:30HRS WENZAKE WATANO WALIFIKA ENEO HILO NDIPO ASKARI WALIPOWAAMURU
WAJISALIMISHE WALIKAIDI AMRI HIYO NA KUANZA KUFYATUA RISASI UWELEKEO WA ASKARI
WALIPO NA ASKARI WAKAJIBU MAPIGO NA KUWEZA KUWAJERUHI MAJAMBAZI WAWILI TAJWA
HAPO JUU NA ZILE RISASI WALIZOZIPIGA ZILIWEZA KUMJERUHI MWENZAO ALIYEKUWA
AMEPELEKA ASKARI KWENYE ENEO LILE, WOTE WATATU WALIFARIKI DUNIA WAKATI
WANAPELEKWA HOSPITALI KWA MATIBABU.
KATIKA ENEO LA TUKIO POLISI WALIFANIKIWA KUIPATA
SILAHA BASTOLA HIYO DUTY CZ 75P-07 TAJWA HAPO JUU ILIYOKUWA
IMEPORWA/KUNYANG’ANYWA KULE NYAMONGOLO MALI YA SULEIMANI WAZIRI ALIYEKUWA
ANAMILIKI KIHALALI NA SHORT GUN ILIYOFUTIKA NAMBA. MIILI YA MAJAMBAZI HAO
IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI,
MSAKO WA KUWASAKA WENZAO AMBAO WAMETOROKA NA WENGINE WALIOKUWA WANASHIRIKIANA
NAO BADO UNAENDELEA. KATIKA UPELELEZI WA AWALI MAJAMBAZI HAWA NA WENZAO
WAMEKUWA WAKIFANYA MATUKIO YA UVUNJAJI WA NYUMBA USIKU NA KUFANYA UNYANG’ANYI
NA KUBAKA PINDI WANAPOVUNJA NYUMBA ZA WATU USIKU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA
POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWAOMBA
KUENDELEA KUTOA TAARIFA SAHIHI NA MAPEMA ZA WAHALIFU/UHALIFU KWANI WANAWAFAHAMU
NA PIA NI VIJANA WAO AMBAO WANAISHI NAO KATIKA MAKAZI YAO, ILI POLISI WAWEZE
KUWAKAMATA KABLA HAWAJALETA MADHARA MAKUBWA KWA WANANCHI, PIA ANAWASHAURI
VIJANA WAFANYE KAZI HALALI ZA KUJIPATIA KIPATO WAACHANE NA TABIA YA KUJIHUSISHA
NA VITENDO VYA UJAMBAZI KWANI VITAGHARIMU MAISHA YAO.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
No comments:
Post a Comment