Disemba 05 na 06 mwaka huu 2016 ulifanyika Mkutano Mkuu wa Waendeshaji/
Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii nchini kupitia umoja wao wa Tanzania Bloggers
Network TBN, uliofanyika ukumbi wa PSPF Jijini Dar es salaam.
Siku ya kwanza ilikuwa mahususi kwa ajili ya semina kwa wanablogu hao juu
ya namna ya kuendesha mitandao yao kwa ajili ya manufaa ya kijamii na yao pia.
Siku ya pili ilikuwa mahususi kwa ajili ya mkutano Mkuu ambapo wajumbe wa
mkutano huo waliwachagua viongozi wao ambapo Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi
(aliyesimama juu) na wasaidizi wake walisalia katika nafasi zao.
#BMGHabari
Mkutano huo ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Idara
ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, ambapo alitamka
rasmi kwamba serikali inatambua mchango wa wanablogu nchini katika kuipasha
jamii habari hivyo itaendelea kushirikiana nao akionya watendaji wa serikali
hususani maafisa habari wa mikoni wasiotoa ushirikiano kwa wanablogu hao kuacha
mara moja tabia hiyo.
Katika kilele cha mkutano huo, mgeni rasmi alikuwa
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye, ambaye alikiri
umuhimu wa wanablogu nchini akisema kwamba, watatambuliwa rasmi kupitia kanuni
za sheria mpya ya vyombo vya habari nchini ya mwaka 2016 na kwamba watapewa
kadi za wanahabari (Press Card) ili kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi.
Kauli iliyowafurahisha wengi ni ile ya Waziri Nnauye
aliyowakaribisha wadau mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa tuzo kwa wanablogu
kwa mwaka ujao 2017 akisema wanafanya kazi kubwa hivyo ni vyema kutambua
mchango wao kupitia tuzo.
BMG inawapongeza wote waliofanikisha mkutano huo,
ikiwemo Bank ya NMB kwa ufadhiri wake, NHIF, PSPF, Kampuni ya bia Serengeti,
Cocacola na TANAPA. Kwa pamoja tuienzi kaulimbiu ya mkutano huo, “Mitandao
ya Kijamii ni Ajira, Itumike kwa Manufaa”.
Kutoka kushoto ni Katibu wa TBN, Khadija
Kalili, Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo Dk. Hassan Abbas na Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na
Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili na mjumbe wa kamati tendaji TBN, Klantz
Mwantepele.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa
Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Katikati ni
Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi na kushoto ni Katibu wa TBN, Khadija Kalili.
Mwanablogu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya
wenzake
No comments:
Post a Comment