Saturday, December 10, 2016

TAKUKURU BAGAMOYO, WAADHIMISHA SIKU YA MAADILI.

Wa kwanza kushoto ni mkuu wa TAKUKURU wilaya ya  Bagamoyo, Raymond  Kitima, wa pili  kushoto ni Makamo mkuu  wa Chuo  kikuu cha  Marian, (MARUCO)  Dkt.  Zakayo  Kimaro. kutoka kulia wa kwanza ni Mkuu  wa  Polisi  wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu  Mwandamizi  wa  Polisi, SSP- Adam  Maro, na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatma Omari Latu.
..........................................................
Taasisi ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa Nchini TAKUKURU wilaya ya  Bagamoyo imeadhimisha siku ya maadili duniani, ambapo wilaya ya Bagamoyo imefanyika katika Chuo  Kikuu cha  Marian University College  (MARUCO).

Katika Maadhimisho hayo  uliendeshwa Mdahalo wa kujadili mmomonyoko  wa maadili katika Jamii  hali inayopelekea kichocheo cha rushwa kwa vijana.

Watoa mada mbalimbali walieleza  namna jamii  ilivyotoka kwenye maadili mema kuanzia ngazi ya familia na hatimae taifa  kwa ujumla hali inayosababisha kuwepo kwa Rushwa katika kila sekta  bilaya  kuwa na hofu yoyote.

Aidha, imeelezwa kuwa, tamaa ya kupata mafanikio kwa haraka ni  miongoni  mwa vichocheo vinavyopelekea rushwa kwakuwa kila  mwenye nafasi fulani katika kazihuona njiapekee yakupatya  mafanikio ni   kupokea rushwa.

Mdahalo huo uliowajumuisha wanafunzi kutoka vyuo vya  TaSuBa, ADEM, MARUCO NA SLADS Washiriki walitaka baadhi ya sheria katika maeneo mbalimbali zifanyiwe marekebisho  ili kupunguza  urasimu  katika mambo maeneo mbalimbali ya kupata huduma ambayo kwa kiasi  kikubwa huchangia  vitendo vya Rushwa.

Kwa upande wao viongozi wa  dini  wameitaka jamii  kurudi kwenye mafundisho ya dini  zao ili waweze kuwa n a Hofu juu ya  Mungu ambapo wataweza mkusimamia haki na kupinga Rushwa kwakuwa  vitendo vya Rushwa vinapingana na upatikanaji wa haki  kwa mwenye haki.

Mkuu  wa Taasisi ya  Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wialaya ya Bagamoyo, Raymond Katima,  aliwataka wananchi wilayani  Bagamoyo kutoa ushirikiano na Taasisi ya  kuzuia na  kupambana na Rushwa ili kufichua vitendo  vya hivyo.

Alisema Rushwa ina miziz mingi katika jamii tatizo na  kwa kiasi gani vitendo hivyo vinaripotiwa ili viweze kushughulikiwa kisheria.

Aidha,  aliwataka wanafunzi  kuweka bayana namna  Rushwa ya  ngono   ilivyotawala  katika vyuo  mbalimbali  wilayani Bagamoyo na  kwamba  iki bainika hatua zichukuliwe dhidi ya muhusika.

Aliongeza kuwa jamii  imeathirika na vitendovya Rushwa na  kupelekea hata   paleunapomuhudumia kwa moyo mmoja akili yake haimini kama umemuhudumia na kuanza kuteneza  mazingira ya kukupa Rushwa yeye  mwenyewe  bila ya  kuomb wa hali ambayo inarudisha nyuma mapambano dhidi ya Rushwa.

Siku ya  maadili duniani huadhimishwa Desemba 10  ambapo kaulimbiuya  mwaka huu ni  Kujenga na kukuza maadili,  Haki za Binadamu, Uwajibikaji,  Utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa.
Dkt. Eligius Mkulima Mhadhiri wa chuo Kikuu cha  Marian (MARUCO) akiwasilisha mada katika Mdahalo huo.
Washiriki wa Mdahalo huo katika siku ya  maadili  wakifuatilia mada zilizowasilishwa.
 Wa kwanza kushoto ni mkuu wa TAKUKURU wilaya ya  Bagamoyo, Raymond  Kitima, wa pili  kushoto ni Makamo mkuu  wa Chuo  kikuu cha  Marian, (MARUCO)  Dkt.  Zakayo  Kimaro. kutoka kulia wa kwanza ni Mkuu  wa  Polisi  wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu  Mwandamizi  wa  Polisi, SSP- Adam  Maro, na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatma Omari Latu.
 Washiriki wa Mdahalo huo katika siku ya  maadili  wakifuatilia mada zilizowasilishwa.
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha  Marian, (MARUCO) Dkt. Samuel Nguni, akiwasilisha mada katika mdahalo huo.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, wakifuatilia Mdahalohuo.
Mtoa mada  katika Mdahalohuo, Endrew Maselele, akiwasilisha mada.
Mkuu wa TAKUKURU Bagamoyo, Raymond Kitima.
 Mkuu wa TAKUKURU Bagamoyo, Raymond Kitima.
 Makamu mkuu wa  Chuo cha Marian Bagamoyo, (MARUCO) Dkt. Zakayo  Kimaro akifunga mdahalo huo.

No comments:

Post a Comment