VEDMA KUCHONGA BARABARA KIMANGE - PONGWE MNAZI

 

VEDMA KUCHONGA BARABARA KIMANGE - PONGWE MNAZI


Na Omary Mngindo, Kimange



KAMPUNI ya Vedma Investment imekabidhiwa Barabara kutoka Kimange mpaka Pongwe Mnazi, Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, iichonge ili ipitike vipindi vyote.


Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) wilayani hapa kupitia Meneja Bupe Angetile, mbele  ya Diwani wa Kata Juma Gurumo akimtambulisha Mkandarasi huyo.


Akizungumza kwenye kikao hicho, Meneja Bupe alisema kuwa wamepokea kiasi cha shilingi milioni 130, zitazojenga Kilometa 12 ambapo kati ya hizo zitatengenezwa 9 zilizosalia kilometa tatu ni zile korofi zitazopewa kipaumbele kikubwa.


"Kwa kiasi tulichonacho tukisema tuweke changarawe yote haitotufikisha popote, tumeona tuweke kipaumbele maeneo korofi ikiwemo kwenye vilima ili tuondoe changamoto zinazotokea kipindi cha mvua," alisema Mhandisi Bupe.


Kwa upande wake Diwani Gurumo alianza kumpongeza Meneja huyo kwa kuweza kumkabidhi Mkandarasi huyo eneo la mradi, kitu ambacho hakijawahi kutokea huku akiwaomba wakazi kuwapatia ushirikiano wakati wa utekeleza wa kazi hiyo.


"Meneja huyo amekuwa na ushirikiano mkubwa katika Halmashauri yetu, binafsi tangu nichaguliwe amekuwa msaada mkubwa, leo tunashuhudua amefika kwa pamoja tumekaua maeneo korofi na ndio tumeweka kipaumbele," alisema Gurumo.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnazi Juma Baruti alishangazwa kwa hatua ya kumuona Mkandarasi kufika kushauliana, kwani kwa miaka mingi wamekuwa wakiona magreda yanachonga tu Barabara pasipo kushirikishwa.


"Leo tunaona maajabu kwani kitu kama hiki cha kukaa na Meneja wa TARURA na Mkanrasi hatujawahi kuiona, zaidi ya kushuhudia Magreda yakichonga Barabara pasipokushirikishwa," alisema Baruti.







Comments

Popular posts from this blog

GURUMO AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA NA WAZIRI KIKWETE

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

RAIS WA ZANZIBAR ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME.

MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA.

TITF YAANDAA TAMASHA LA SANAA ZA UFUNDI ARUSHA

GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA ZAIDI YA BIL 4 IGUNGA

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA