Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam na Makao Makuu
wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari
Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47.
Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam na Makao
Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47.
Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47.
Wachezaji wa kuvuta kamba timu ya Bandari ya Tanga
wakichuana dhidi ya Makao Makuu mchezo umalizika kwa Tanga kuibuka na ushindi
wa seti 2-0 mchezo uliochezwa viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly mjini
Tanga
TIMU ya Mpira wa Pete ya Bandari ya Tanga leo
wameweza kuibuka na ushindi wa mabao 43-16 dhidi ya Bandari ya Mtwara kwenye
michuano ya Bandari inayoendelea mjini Tanga.
Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye viwanja vya
Bandari mjini hapa ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko Bandari Tanga
ilikuwa ikiongozwa kwa mabao 23 -17 dhidi ya Mtwara.
Halikadhalika Tanga wakiweza kuibuka pia na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa mpira wa miguu
uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini hapa.
uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini hapa.
Katika mchezo mwengine uliochezwa kwenye
uwanja huo timu ya Bandari ya Dar es Salaam iliweza kuibuka na ushindi dhidi ya
Makao Makuu kwa mabao 36-13.
Wakati huo huo,Timu ya Bandari ya Dar es
Salaam imeweza kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47 dhidi ya Makao Makuu kwenye
mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye dimba hilo la Bandari mjini hapa.
Kwenye mchezo mpira wa miguu uliozikutanisha
Bandari Mtwara na Maziwa Makuu ambapo timu hizo mpaka dakika 90 zilijikuta
zikigawana pointi moja moja baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Ili kuonyesha wana umahiri mkubwa kwenye
michezo Bandari Tanga wanaume waliweza kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya
Makao Makuu kwenye mchezo wa kuvuta kamba.
Wakati wanaume wakiibuka na ushindi huo
wanawake nao waliweza kuwaunga mkono wenzao kwa kuibuka na ushindi wa seti 2-0
dhidi ya Makao makuu kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja
vya shule ya Sekondari Popatlaly.
Mashindano hayo ambayo yalifunguliwa jana na
Mkurugenzi wa Bandari nchini (TPA) Deusdedit Kakoko ambaye aliwataka
wanamichezo hao kuzingatia nidhamu na maarifa kwenye michezo yao ili kupata
ushindi.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya
Tanga Raha.
No comments:
Post a Comment