Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano
wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula
uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo aliwapongeza
TAFOPA kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini pia aliwataka Wasindikaji kuongeza
ushirikiano ili kufikia maendeleo na mafanikio ya juu.
........................
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa mbalimbali
za vyakula vilivyosindikwa zinazotengenezwa na wajasiriamali muda
mfupi kabla ya kufungua wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya
Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo mbioni
kupunguza muda wa utoaji wa leseni za biashara nchini ili kutoa fursa kwa
wananchi wengi zaidi kupata leseni hizo kwa ajili ya shughuli za kibiashara.
Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati anafungua mkutano wa wadau wa
kuendeleza maeneo tengefu ya viwanda vya usindikaji wa vyakula nchini.
Makamu wa Rais amesema
mpango utaenda pamoja na kupunguza baadhi ya kodi na tozo ambazo ni kero kwa
wananchi hasa wenye viwanda kama hatua ya kukuza biashara na uwekezaji katika
sekta ya viwanda nchini.
Amesisitiza kuwa Serikali
inaendelea na mazungumzo na wenye mabenki hususani benki ya TIB ili kutoa
mikopo yenye riba nafuu kwa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda.
Kuhusu usindikaji wa
bidhaa nchini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe katika
jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kumuwezesha mwanamke kiuchumi
akiwakilisha nchi za ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika amepongeza
jitihada zinazofanywa na wasindikaji wadogo nchini katika utengenezaji wa
bidhaa mbalimbali ambazo zitakidhi katika masoko ya ndani na
nje ya nchi.
nje ya nchi.
“Serikali inafarijika
sana kuona kuwa wasindikaji wadogo nchini wamethubutu na wana uwezo wa
ushindani katika biashara ya ndani na hata nje, hivyo tunayohaki ya kujigamba
kwa kuthubutu, Tumeweza na Tuendelea Kusonga mbele”
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema umefika wakati kwa Wizara
na taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo kuona umuhimu wa kuhakikisha
viwanda vinajengwa vijijini ili mkulima mdogo anapolima awe na uhakika wa
kupata soko katika viwanda hivyo.
Amesema kuwa hali hiyo
itaondoa changamoto ya kusafirisha bidhaa
nyingi ambazo zinaharibika njiani au zinapofika sokoni na hivyo kukosesha jamii kipato kilichotarajiwa.
nyingi ambazo zinaharibika njiani au zinapofika sokoni na hivyo kukosesha jamii kipato kilichotarajiwa.
Makamu wa Rais pia
amehimiza watafiti nchini wajielekeza
katika kufanya tafiti ambazo zitasaidia sekta binafsi na serikali kwa ujumla kuhusu namna bora ya kukuza sekta ya viwanda nchini.
katika kufanya tafiti ambazo zitasaidia sekta binafsi na serikali kwa ujumla kuhusu namna bora ya kukuza sekta ya viwanda nchini.
Kwa upande
wake, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji
Charles Mwijage amekiri kuwa bado kuna changamoto kubwa ya maeneo ya yatakayojengwa viwanda na kwamba Serikali
imeliona tatizo hilo na inalifanyia kazi ambapo tayari imeshaziagiza Halmashauri zote nchini kujenga maeneo kwa ajili ya viwanda.

Wadau waliohudhuria na kushiriki
wakimsikiliza kwa makini Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa TAFOPA Bi. Suzy Laizer
akihutubia wakati
ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya
Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi kwenye mkutano huu alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

No comments:
Post a Comment