Mkuu wailaya ya Bagamoyo akizungumza na mwanafunzi katika shuleya msingi Mbwewe ambae mahudhurio yake Darasani siyo mazuri katika mojaya ziara zake za kutembelea shule zilizopo katika Wilaya yake.
.....................................
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga,
amewaagiza watendaji kata kuandaa mikataba
na wazazi na walezi wote wilayani humo, itakayothibitisha kuwapeleka
watoto wao shule kuanza kidato cha kwanza kwa wale waliofaulu elimu ya msingi.
Kauli hiyo ameitoa kwenye mikutano ya hadhara kwa
nyakati tofauti alipofanya ziara kwenye
kata mbalimbali wilayani humo.
Majid alisema kila mzazi au mlezi anapaswa
kumuandaa mwanae aliyefaulu darasa la
saba ili ampeleke kuanza kidato cha
kwanza mara tu shule zitakapofunguliwa mwezi Januari.
Alisema kila mtendaji wa kata aandae mkataba
ambao mzazi au mlezi atathibitisha kwamba atampeleka mtoto shule kuanza kidato
cha kwanza na kwamba asipompeleka apelekwe mahakamani na mkataba huo usainiwe
na mzazi au mlezi huku mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kijiji wanatakiwa
kusaini kama mashahidi.
Alisema Elimu ndiyo urithi pekee usiofilisika kwa mtoto hivyo kila mzazi
anapaswa kuweka mikakati ya kumsomesha mwanae kwaajili ya faida yake na taifa
kwa ujumla.
Aliongeza kwa kusema kuwa dhamira ya Rais
Dkt. John Magufuli
kuweka sera ya elimu bure hapa nchini ni kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake
ya msingi ya kupata
elimu hivyo wazazi wasiwe sehemu
ya kuwanyima watoto wao haki hiyo.
Aidha, alisema kuwa kufuatia mkakati wa Mheshimiwa
Rais Dkt. John Magufuli wa kutengeneza madawati nchi nzima, katika wilaya
ya Bagamoyo kwa sasa hakuna upungufu wa
madawati baada ya kuwa zoezi la utengenezaji madawati
kukamilika kwa zaidi ya
asilimia mia moja.
Wanafunzi wakiwa wamesongamana kwenye Darasa moja
kutokana na upungufu wa vyumba vya kusomea katika shuleya msingi Kibindu.
Hata hivyo alisema kuwa zipo baadhiya shule
zinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayopelekea watotokukaa Darasani kwa msongamano, na kwamba tayari ameweka
mikakati ya kiwilaya kuhakikisha changamoto hiyo inaondoka.
Alisema amewaagiza watendaji wa kata kwa
kushirikiana na wenyeviti wa vijiji na watendaji wa vijiji kuangalia mahitaji
ya vyumba vya madarasa katika maeneo yao nu
kuweka mikakati ya kujenga
madarasa ili kuondoa tatizo la madarasa.
Akizungumzia mkakati huo wa ujenzi wa madarasa kwa wilaya ya Bagamoyo, alisema kuwa unakwenda vizuri ambapo kila kata yenye upungufu wa madarasa
imeanza kutekeleza ujenzi wa madarasa
kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika wakiongozwa na
madiwani wao.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid
Mwanga menye fulana nyukundu akiwa juu ya jengo la darasa shuleya msingi
Kibindu.
Mkuu huyo wa wilaya ya Bagamoyo
ametoa wito kwa wadau wa elimu kuchangia
ujenzi wa madarasa katika wilaya hiyo ili kuondoa upungufu wa vyumba vya
madarasa.
Alisema mahitaji ni vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo, Saruji, Mabati, Nondo huku wananchi akiwataka kujitolea nguvu zao kufanikisha ujenzi huo wa madarasa katika kata mbalimbali wilayani bagamoyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majidi Mwanga,
akizungumza na wanafunzi wa shule ya
msingi Kiwangwa katika moja ya ziara
zake wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, akizungumza na
wanafunzi wa shule ya Sekondari Kiwangwa katika moja ya Ziara zake ndani ya
wilaya yake.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akiwa
katika shule ya msingi Mapinga katika moja ya ziara zake wilayani humo.
Mkuu wa wilayaya Bagamoyo, Majid Mwanga
akizungumza na watoto wa jamii ya wafugaji ambao hawajapelekwa shule katika
kata ya Ubena alipofanya ziara yake
katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akipata maelezo ya
kwanini watoto hawaendi shule
kutoka kwa kina mama wa jamii ya
wafugaji, kata ya Ubena katika moja ya ziara zake wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid mwanga akiwa
katika shule ya msingi Fukayosi kata ya Fukayosi.
PICHA ZOTE KUTOKA MAKTABA YA BAGAMOYO KWANZA BLOG.
No comments:
Post a Comment