Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mkoani Pwani, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi
wa kijiji cha Kibuyuni Kata Panzuo baada kufunga barabara kwa lengo la
kufikisha malalamiko yao.
Mkazi wa kijiji cha Kibuyuni Kata Panzuo,Juma Mwengele akizungumza
kwaniaba ya wananchi wezake wa Kata ya Panzuo juu ya Ng’ombe ambao
wanapita kuharibu vyanzo vya Maji na hata mazao.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ,Abdallah Ulega akikagua timu kabla ya
mchezo wa Kombe la Ulega Cup.
...........................
WANANCHI wa Kata ya Panzuo wamelazimika kufunga barabara kwa lengo la
kufikisha malalamiko yao Kwa Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega ambaye
Alikuwa anatoka kijiji cha mkuruwili, kusikiliza kero yao hususani Ng’ombe ambao
wamekuwa tatizo kubwa katika Wilaya ya Mkuranga.
Wananchi hao ambao walilazimika kukaa katikati ya barabara walimweleza Mbunge Ulega kwamba wanataka kusikia kauli yake juu ya uharibufu unaofanywa na Ng’ombe hao.
Akizungumza kwaniaba ya wananchi wezake Mkazi wa kijiji hicho Juma Mwengele alisema kuwa wamelazimika kufunga barabara ili kuonesha hisia zao kwamba wanakerwa na uharibufu unaofanywa na Ng’ombe ambao wanapita kuharibu vyanzo vya Maji na hata mazao.
“Ndugu mbunge kwaza tunaomba samahani sana Kwa kuharibu utaratibu wako lakini tumeladhimika kufanya hivyo kutokana na wanyama wanaitwa ng’ombe,kwakweli wanatuasili mno na tuseme tu hatuwataki sisi.”alisema Mwengele.
Aliongeza kuwa ng’ombe wamekuwa tatizo kubwa na kadri siku zinavyokwenda hali inazidi kuwa mbaya mno kwani wanyama hao kila siku wanaingia Kwenye maeneo muhimu hususani kwenye vyanzo vya Maji pamoja na mashambani.
No comments:
Post a Comment