Saturday, December 10, 2016

WAHITIMU WA MAFUNZO YA MGAMBO BAGAMOYO KUPATIWA AJIRA JKT.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid HemedMwanga, akizungumza  wakati wakufunga mafunzo ya  Mgambo, kata ya Mapinga.

Vijana 102 waliohitimu mafunzo ya  Mgambo kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo, wamepata  Ajira Jeshi  la  Kujenga Taifa, JKT.

Akifunga mafunzo hayo ya mgambo, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga, alisema mgambo hao tayari wamefa nyiwautaratibu wa kupata Ajira kupitia jeshi  la Kujenga Taifa JKT, ili kuondoa changamoto ya ajira ambayo inawakabili vijana wengi hapa nchini.

Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais, Dkt. John Magufuli, imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha inaondoa tatizo la Ajira  kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea mazingira rafiki ya kuajiriwa na kujiajiri.

Majid, Alisema katika  kukabiliana na changamoto ya ajira,  wilayani Bagamoyo Bagamoyo tayari kuna viwanda vitatu vinavyotarajiwa kufunguliwa wakati wowote ili kutoa fursa kwa vijana  kupata ajira.

Alifafan ua  kuwa, Kata ya Mapinga kuna  Kiwanda c ha kusindika Matunda cha Elvin ambacho kitatoa fursa kwa watu watakaolima matunda mbalimbali ikiwemo manasi, maembe, Nyanya nk. kwenda kuyauza na kujiongezea kipato ambapo matunda hayo yatakaushwa na kwenda kuuzwa nje ya nchi.

Aidha, alisema Kiwanda cha pili ni kiwanda cha Sayona  kilichopo  kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze ambacho kitanunua matunda ya Manansi Maembe kwaajili ya kutengeneza juisi na kuongeza kuwa kiwanda cha tatu ni kiwanda cha kusndika Pilipili kilichopo kata ya Kisutu Bagamoyo mjini na kwamba pilipili aina zote zitapata soko katika Kiwanda hicho.

Majid aliwataka wahitimu wa mafunzo ya mgambo kuheshimu sheria za nchi na kulinda kiapo chao ili wasitumike  vibaya  na kusababisha uhalifu.

Alisema kila mgambo anapaswa kuchunga misingi ya sheria za nchi na atakaekiuka na kufanya uhalifu kwa namna yoyote ile atakuwa amevnja  katiba na  kukiuka kiapo chake na kwamba atastahiki kuchukuliwa hatua.

Wakati huohuo amewaonya wawekezaji katika wilaya ya Bagamoyo kuacha kuwanyanyasa mgambo na badala yake kila mgambo anapaswa kuwa na mkataba utakaomlinda  kimaslahi  katika  kufanya kazi yake.

Aidha, aliwataka wawekezaji katika wilaya ya Bagamoyo kuajiri mgambo waliopata mafunzo ili kujiwekea ulinzi wenye uhakika wao na mali zao.

 Baadhi ya wahitimu wa mafunzoya mgambo kata ya Mapinga wilayani  Bagamoyo
 Mshauri wa mgambo wilaya ya Bagamoyo, Meja Iddi Musira katikati akifurahia jambo   mara baada ya kumaliza sherehe za  kufunga mafunzoya  mgambo kata ya  Mapinga.
 MG. Hilda Msaki akizun gumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza mafunzo hayo ya mgambo.


No comments:

Post a Comment