Friday, December 2, 2016

DC BAGAMOYO AMPA SIKU MOJA OCD CHALINZE KUMUHAMISHA MKUU WAKITUO CHA WAMI KWA KUTOSHUGHULIKIA MATATIZO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA.

Mkuu  wa wilaya ya Bagamoyo, Majid  Mwanga  amempa siku moja kamanda wa polisi wilaya ya  Kipolisi Chalinze SSP Janeth Magomi, kumuondoa mkuu wa kituo cha  polisi cha Wami kufuatia tuhuma za  kuwapendelea wafugaji na kuwanyanyasa  wakulima na  kupelekea  kushindwa kuwachukulia hatua wafugaji wanaoingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima.

Agiza hilo  amelitoa kwenye  Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha  Mandela kata ya Mandela ambapo awali wananchi  walipata nafasi ya kutoa  malalamiko yao  mbele ya mkuu wa wilaya na kufanya kero  kubwa iliyotawala katika mkutano huo ni kuhusu wafugaji  kuingiza mifugo  kwenye  mazao ya  wakulima na kwamba polisi waliopo kituo cha  polisi Wami wameshindwa kuwasimamia ili kudhibiti hali hiyo.
Akizungumza mbele ya  mkuu  wa wilaya mzee mmoja  alisema aliwahi kufika kituo cha    PolisiWami kutoa Taarifa ya kuliwa mazao yake,  lakini hatua  waliyochukua  Polisi ni  kumwambia huyo mzee akatafute mgambo ili  amkamate mfugaji aliyeingiza mifugo kwenye shamba  lake jambo  limemsikitisha mzee huyo.

Aidha, wananchi mbalimbali walizungumza  katika mkutano huo, wamelalamikia kitendo cha wafugajikuwa na uwezo wa kuharibu mazao ya wakulima bila ya kuchukuliwahatua yoyote.

Kero hizo za wafugaji kwa wakulima ni pamoja na mifugo kula mazao  ya wakulima na hata wanapotakiwa kutoa fidia ya mazao hayo  wamekuwa hawatimizi  kwa kile kinachodaiwa kulindwa na  Polisi, mkuu wa wilaya   anachukua jukumu  la kuomba namba za simu za wafugaji wanaodaiwa na wakulima na kuwapigia simu ili walipe fidia za wakulima.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Kipolisi Chalinze. Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Janeth Magomi akimsikiliza  mkuu  wa wilaya wakati wa mkutano  uliofanyika  kijiji cha Mandela  kata ya Mandela Halmashauri ya Chalinze,  kulia ni mkuu  wa kituo cha Polisi  Wami ambae mkuu  wa wilaya ameagiza ahamishwe.
Wazee wa Kijiji cha  Mandela  wakipiga makofi mara baada ya  mkuu  wa wilaya kutoamaamuzi ya kuhamishwa kwa mkuu wa kituo cha  polisi Wami.
Wananchi wa kijiji cha Mandela wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga alipofanya mkutano wa hadhara na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi  wa  kata ya Mandela, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.

1 comment:

  1. Ni vema kuwachukulia hatua wafugaji. Wameharibu pia Ruvu Japanese financed improved rice irrigation system majaruba yamejaa mifugo pia mifereji ya umwagiliaji imeharibiwa. Wakulima ambao wengine wazee wanatoka bagamoyo mjini na wengine wanaishi hapo Makurunge, wakilima toka wengine hatujazaliwa sasa wazee. Wanalishia mashamba Morogoro Rural hata kule walikopewa kukaa mbali na mashamba na makazi ya wakulima bado wanatoka huko mbali kwunda kulisha mifugo yao mashamba ya wakulima. Wanachanga hela kwa kuuza ng'ombe, mbuzi wanahonga police hela nyingi. Police mishahara midogo wana njaa wanachukua rushwa. Mikumi Moran alilishia mifugo shamba, mama mtu mzima akaenda kuifukuza, akachapwa, akabakwa. alilazwa hospitali mume kwenda kuambiwa yaliyomfika mama alianguka akafariki-alipata mshtuko. Mama huyo kwa bahati nzuri alimvuta chini huyo moran akavimba. Alipokwenda hospitali kutibiwa St Kizitoi Health Centre alipolazwa muathirika-aliitwa kumtambua, akamtambua na alimwimbia simu akakutwa nayo akakamatwa. Cha kushangaza-alitorokea alipowekwa kolokoloni kituo cha polisi Mikumi. Mama amepata kilema, kulima tena hawezi, baba/mumewe kafariki na Mmasai mbakaji-katorokea police post!? Ndio maana police wana mavitambi-rushwa!Wakulima wanaamua kukata mapanga mifugo na kuchoma moto mabanda ya wafugaji.

    ReplyDelete