Raia wa Ethiopia
81 wamekamatwa Bagamoyo wakiwa katika katika harakati za kusafirishwa kupitia usafiri
wa Baharini.
Akitoa Taarifa
kwa waandishi wa Habari mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Mwanga, alisema watu hao wamekamatwa kufuatia ushirikiano na raia wema ambao
walitoa taarifa polisi na kufanikisha kuwakamata
watu hao ambao wameingia nchini bila ya kufuata sheria.
Alisema
tukio hilo limetokea leo
Tarehe 10 Desemba,
kitongoji cha Mjimpya kata ya Kisutu katika eneo la kingani ambapo watu hao
walikutwa hapo.
Alisema vyombo vya ulinzi wilayani
Bagamoyo vimejipanga kukomesha
vitendo vyote vya kihalifu ikiwa ni pamoj a upitishaji wa biashara za magendo na
wahamiaji haramu.
Aidha,
aliwataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na Usalama
ili kufichua maovu mbalimbali yanayofanyika katika wilaya
ya Bagamoyo.
Akizungumzia
madhara ya kuwaficha wahamiaji haramu ni
pamoja na kukithiri kwa vitendo
vya kihalifu na kuambukizana magonjwa kutokana na kuwa waliongia bilaya vibali hawakupitia kwenye ngazi za
kuwahakiki ikiwa wana magonjwa ya kuambukiza au
la.
Mmoja wa
wahamiaji hao Shemsadin Wesorow, akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema wametokea katika Nchi ya Ethiopia lengo
likiwa ni kwenda Afrika ya
Kusini kufanya kazi na kwamba hawakutoroka kutoka kwao.
Alisema
alipigiwa simu na kaka yake ambae anamiliki Duka kubwa huko
Afrika ya kusini ili aende
nae akapate kazi.
Akizungumzia ni kwa namna gani wangeweza kuishi huko hali ya wako wengi,
Shemsadini alisema kila mmoja
kati yao ana ndugu huko kwahiyo
isingekuwa tabu kuishi huko.
Alipoulizwa kuhusu idadi kamili katika msafara wao alisema wametoka 93 lakini waliokamatwa na polisi ni 81 tu na 12 waliobaki wamekimbilia
vichakani.
Aidha, ameiomba
serikali ya Tanzania iwasaidie kurudi
nchini kwao na kwani baadhi yao
wamechoka kwa njaa huku wengine wakiwa
wanaumwa bila ya kupata matibabu
kutokana na mazingira ya kujificha katika safari yao.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
No comments:
Post a Comment