MAMLAKA ya
Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya
umeme kwa asilimia 8.5%.
Kwa mujibu
wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani), ongezeko hilo la bei
ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi
EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.
Akitangaza
bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema, baada
ya kufanya uchambuzi wa kina,
Mamlaka
yake imefikia uamuzi wa kuongeza
asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.
asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.
Shirika la
umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa
kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.
Hata hivyo
ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi
uniti 75 kwa mwezi.
Kundi laTIB
linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo
ya mwezi ya shilingi 5,520.
Shirika la
Umeme Tanzania, (TANESCO), linaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya
umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za
umeme nchini.
No comments:
Post a Comment