Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo, akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga, kata ya Vigwaza, Halmashauriya Chalinze wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa mkoa wa
Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo, akizungumza na wananchi katika mkutano huo, waliokaa chini, wa kwanza kulia ni
Diwani wa kata ya Vigwaza, Muhsini Baruani, na
wa pili ni Mbu nge wa Jimbo
la Chalinze, Ridhiwani Kikwete .
.................................
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo, ametoa siku 30 kwa
wafugaji waliohamia mkoani humo kuondoka baada ya kushamiri kwa migogoro ya
wafugaji na wakulima.
Kauli hiyo aliitoa katika Mkutano
wa Hadhara uliofanyika kijiji cha
Kitonga kata ya Vigwaza katika Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo.
Alisema Serikali haiwezi kufum
bia macho ikiona kila siku vurugu za wafugaji na wakulima ambazo kimsingi
wanaosababisha ni wafugaji wahamiaji ambao sio wenyeji wa mkoa huo.
Mhandisi Ndikilo alisema kila mfugaji anajiona alihamia mkoani
Pwani arudi alikotoka na wala hapaswi kuuliza aende wapi hali ya kuwa
alipoingia mkoani humo aliingia bila
ya kukaribishwa.
Wakati huohuo, Mkuu wa mkoa Ndikilo
amewaagiza wakuu wa wilaya wote
mkoani humo, kusimamia zoezi la kuwaondoa wafugaji hao na kuacha mkoa
ukiwa salama.
Aidha, ameonya wale wote
watakaokaidi amri hiyo hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake.
Migogoro ya wafugaji na wakulima
mkoani Pwani, imekuwa ikiongezeka
kila siku hali inayopelekea machafukoya mara kwa mara na hata mauaji kwa kile kinachodaiwa
kuwa ni jeuri inayofanywa na wafugaji
kwa kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulimana kuharibu mazao.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo, kulia ni mbunge wa Jimbo la
Chalinze, Ridhiwani Kikwete, wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Bagamoyo, Fatuma Omari Latu, na
wapili kushoto ni mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid
Hemed Mwanga.
wanakijiji
cha Kitoga wakisikiliza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na
wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji, Majid Hemed Mwanga akizungumza katika mkutano wa
kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji, kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza
katikaHalmashauriya Chalinze wilayani Bagamoyo.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji, Majid Hemed Mwanga akizungumza katika mkutano wa
kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji, kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza
katikaHalmashauriya Chalinze wilayani Bagamoyo.
Watumishi wa Halmashauri ya Chalinze wakifuatilia
mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, mwenye
miwani, akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu,
aliyevaa shati la Kitenge katikati ni
Mkurugenzi wa HalmashauriyaChalinze, Edesi Lukoa.
No comments:
Post a Comment