Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na watu wenye Ulemavu, Mh. Jensta Mhagama kulia, akipokea Taarifa ya ujenzi wa soko la nafaka lililopo Kitongoji cha Maji coast, kata ya Magomeni, Bagamoyo mjini, katikati ni Mhandisi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Henrico Shauri, na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Najid Mwanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Ajira na watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista
Mhagama amemuagiza Mhandisi wa Halmashuri ya Bagamoyo, Henrico Shauri,
kukamilisha kazi zilizobaki ndani ya
wiki mbili ili Soko hilo liweze kufunguliwa mwezi January 2017.
Waziri Jenista Mhagama alitoa agizo hilo alipotembelea
ujenzi wa soko hilo ambapo
ameridhishwa na shughuli za ujenzi zilivyoenda na kusema kuwa hakuna sababu ya
kuchelewa kulifungua soko hilo ili wananchi waweze kufaidika na uwepo wa soko
hilo.
Alisema mpaka kufikia Tarehe 30 mwezi Desemba
kila kitu kiwe kimekamilika ili mwezi January
liweze kufunguliwa, ambapo waziri mkuu anatarajiwa kulifungua soko hilo.
No comments:
Post a Comment