Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, akikabidhi Hundi ya
shilingi Milioni 3 kwa kikundi cha Jipe moyo kilichopo kijiji
cha Hondogo Halmashauri ya
Chalinze.
Mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, Majid Mwanga akikabidhi
Hundi ya shilingi milioni 2 kwa
kikundi cha Umoja ni Nguvu kilichopo kijiji cha Lupungwi.
.....................................
Halmashauri ya Chalinze imegawa fedha za kina mama na vijana ili kujiendeleza
katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Akizungumza
kabla kukabidhi hundi kwa vikundi
vya Jipe Moyo na Umoja ni nguvu, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga alisema vikundi vyote vilivyopata fedha hizo
vinapaswa kuziingiza kwenye miradi
mbalimbali ili wazirejeshe kwaajili ya kuendelea na mgao kwa vikundi vingine.
Alisema fedha hizo zimetokana na asilimia10
inayotengwa katika Halmashauri kwaajili
kina mama na vijana ambapo Halmashauri ya Bagamoyo imetenga shilingi
milioni 126 na Halmashauri ya Chalinze imetenga milioni 79.
Aidha, mkuu huyo wa wilaya aliwasifu wakurugenzi
wa Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze kwa
kusimamia vyema mapato na kuwapongeza madiwani kwa
kusimamia asilimia kumi kwaajili ya kina mama na vijana.
Katika mgao huo kikundi cha Jipe moyo kutoka
kijiji cha Hondogo, kimepata shilingi milioni 3 na kikundi cha Umoja ni Nguvu kutoka kijiji cha Lupungwi
kimepata milioni 2.
No comments:
Post a Comment