Makamu
wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili
kushoto akishiriki mazoezi ya viungo katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya
kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasioambukiza nchini uliofanyika leo
jijini Dar es salaam kushoto ni Rais Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Alhaji Ally
Hassan Mwinyi,wa pili kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangalla kulia .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na
wananchi kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi katika uzinduzi wa kampeni ya
kitaifa ya kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasioambukiza nchini
uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
...................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan amewataka wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuandaa siku ya mazoezi ya
hiari kila ifikapo jumamosi ya pili kila mwezi ili kuepuka magonjwa
yasioambukiza.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi Mhe.
Samia Suluhu amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuandaa utaratibu wa mazoezi
pamoja na wananchi kila mwezi ili kuweka jitihada za kukinga magonjwa hayo.
“Watanzania tupende kufanya mazoezi mara kwa mara ili tuweze kuepuka
magonjwa yasioambukiza yakiwemo Kisukari, magonjwa ya moyo, saratani ambayo
yanasababishwa na mafuta mengi mwilini ”alisema Mhe. Suluhu.
Aidha Mhe. Samia amewaagiza wakuu wa Mikoa na Halmashauri kurudisha
viwanja vyote vya michezo vilivyovamiwa ili watu wapate kufanya mazoezi na
wasiokua na viwanja watafute maeneo kwa ajili ya shughuli hiyo.
Mbali na hayo Mhe. Samia amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu nchini
kuandaa mpango endelevu na viwanja vya michezo kwa wanafunzi ili kuendeleza
kampeni hii kuanzia mashuleni kwa ajili ya kujenga msingi bora wa michezo.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa asilimia 27 ya vifo vinavyotokea
nchini vinasababishwa na magonjwa yasioambukiza.
Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa mkakati huo ukifanikiwa na kuwafanya
wananchi kuwa na tabia ya kufanya mazoezi utasaidia Serikali kuokoa fedha
nyingi zinazoelekezwa kwenye tiba pamoja na kuokoa maisha ya watanzania wengi
kutokana na magonjwa hayo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi amesema kuwa
mazoezi ni ya maana sana katika kujenga mwili wa binadamu na nguvu kazi ya
taifa kwa maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla.
Mbali na hayo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.
Annastazia Wambura amesema kuna haja ya vifaa vya michezo kushuka bei ili
kuwawezesha wananchi kumudu gharama kwa ajili ya kushiriki michezo.
Aidha Bi. Wambura ametoa onyo kwa mtu au kampuni yeyote kuuza vifaa vya
michezo vilivyoandikwa “HAVIUZWI” ili kuweka urahisi wa wananchi kufanya
mazoezi kwa wingi nchini.
Kampeni hiyo ya kufanya mazoezi ilioandaliwa na Wizara ya Afya
imezinduliwa rasmi leo ili kupambana na magonjwa yasioambukiza kama vile
kisukari, Shinikizo la Damu, uzito uliozidi kiasi , utapia mlo na magonjwa ya
moyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili
kulia akiwaongoza Rais Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi
katikati, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu kulia na Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangalla kushoto na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutembea kutoka viwanja vya leaders hadi
Biafra katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi ili kuepuka
magonjwa yasioambukiza nchini uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati
akiwaongoza baadhi ya viongozi wa kitaifa na wananchi kufanya mazoezi katika
uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa
yasioambukiza nchini uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati
akiwa katika picha ya pampoja baadhi ya viongozi wa kitaifa na wananchi
walioshiriki kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi ili
kuepuka magonjwa yasioambukiza nchini uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati
akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa taifa na kamati ya
magonjwa yasioambukiza (NCD) walioshiriki kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa
ya kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasioambukiza nchini uliofanyika leo
jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment