Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed
Mwanga, leo Tarehe 09 Desemba 2016 amezindua rasmi kilimo katika shamba la Chama cha Ushirika Ruvu, (CHAURU) kwa
msimu wakilimo kwa mwaka 2016/17.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mkuu huyo wa wilaya aliwataka CHAURU
kuanzisha utaratibu wa kuuza mchele badala ya mpunga ili kupata soko kwa
urahisi na kupunguza mfumuko wa bei ya Mchele katika Halmashauri ya Chalinze.
Alisema kutokana na uchaguzi mzuri wa mbegu
inayotum ika katika mashamba hayo, mchele unaolimwa CHAURU umekuwa mzuri na
kwamba unao uwezo wa kuingizwa kwenye ushindani
wa kibiashara.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, akizungumza katika Mashamba ya Chama cha Ushirika Ruvu (CHAURU)
Baadhi ya Matrekta yaliyokuwa yakizindua kilimo katika Mashamba ya CHAURU.
No comments:
Post a Comment