Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuutaarifu
umma kuwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) iliingiza nchini maboksi kumi
na moja (11) ya vitabu/kamusi kutoka nchini Japani kwa ajili ya matumizi ya
elimu.
Kwa mujibu wa sheria ya forodha ya Afrika Mashariki
(The East African Community Customs Management Act, 2004), pamoja na
Sheria ya Ongezeko la Thamani (VAT Act, 2015), vitabu hivi havitozwi kodi ya
forodha wala ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Vitabu hivi vililipishwa tozo ya uondoshaji mizigo
bandarini (Customs Processing fees) shilingi 42,483 na tozo ya Maendeleo
ya Reli (Railway Development Levy) shilingi 106,438 ikiwa ni jumla ya
shilingi 148,921. Baada ya malipo hayo kufanyika, vitabu hivyo vilichukuliwa na
WAMA tangu tarehe 10 , 2016.
Tunapenda kutoa ufafanuzi kwamba taarifa
zilizoandikwa na baadhi ya magazeti hivi karibuni juu ya vitabu hivyo kuwamo
katika orodha ya bidhaa zinazopaswa kupigwa mnada kwa sababu ya kutolipiwa kodi
siyo sahihi.
Kwa kuwa vitabu hivyo havikupaswa kulipiwa kodi ya
Forodha wala VAT kwa mujibu wa sheria, ni wazi kuwa WAMA hawakupaswa kuomba
msamaha wa kodi kwenye Mamlaka yoyote ile.
Orodha iliyowahi kuchapishwa
na baadhi ya magazeti hapa nchini na ambayo ilijumuisha jina la WAMA haikuwa
sahihi.
Pamoja Tunajenga Taifa Letu
1.
J. Kidata
KAMISHNA MKUU
No comments:
Post a Comment